
Josh mwenye umri wa miaka 27 ambaye alicheza Atlanta Hawks kwa muda wa miaka tisa amesaini kuichezea pistons kwa miaka minne ambapo atalipwa jumla ya dola milioni 56 katika kipindi chote hicho .

Josh ni mmoja kati ya wachezaji wachache walioingia kwneye NBA wakitokea shule ya sekondari tofauti na wachezaji wengine ambao mara nyingi huanzia vyuoni kwenye shindano maarufu la kukuza vipaji vinavyokuja kufanya vizuri kwenye NBA la NCAA ambapo alisajiliwa na Atlanta Hawks akitokea shule ya sekondari ya Oakhill Academy huko Atlanta .
Kwa muda mrefu Josh ambaye anafahamika kwa jina utani la J-Smoove alikuwa mchezaji bora kwenye timu ya Atlanta Hawks na ujio wake ndani ya Detroit utaiongezea nguvu timu hiyo ambapo anatarajiwa kuungana na wachezaji kama Andre Drummond na Gregg Monroe huku Atlanta Hawks alikoondoka akirithiwa na Paul Millsapp ambaye amesajiliwa toka Utah Jazz.
No comments:
Post a Comment