facebook likes

Tuesday, July 9, 2013

Barcelona wafikia makubaliano ya kumuuza striker huyu.


david_villa_barca
Taarifa zilizoibuka kwenye mitandao kadhaa ya vyombo vya habari nchini Hispania zinadai kuwa Klabu za Fc Barcelona na Atletico Madrid zimefikia makubaliano juu ya mshambuliaji David Villa . Makubaliano haya ambayo ni ya kimsingi yasiyo rasmi yatamshuhudia David Villa akijiunga na Atletico kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni tano ambapo Madrid watalipa euro milioni mbili kwa mkupuo wa kwanza , Euro milioni mbili nyingine endapo Villa atabakia na timu hiyo msimu ujao na ziada ya Euro milioni moja endapo atakuwepo kwa msimu wa pili. Pamoja na mauzo hayo Barca watakuwa na haki ya kuvuna asilimia hasmini ya fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo ya mchezaji huyo endapo Atletico itaamua kumuuza .
david_villa_lujoso04
Villa amekuwa kwenye wakati mgumu ndani ya kikosi cha Barcelona ambapo ameshindwa kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza hali inayomlazimu kwenda mahali kwingine . Villa ana malengo ya kuwemo kwenye kikosi kitakachoiwakilisha Hispania kwenye michuano ya kombe la dunia mwakani huko nchini Brazil hali inayoleta ulazima wa kuondoka kwake ili azidi kumshawishi kocha Vicente Del Bosque kumuweka kwenye mipango yake ya kombe la dunia .
Villa alijiunga na Barca akitokea Valencia misimu mitatu iliyopita ambapo alinunuliwa kwa zaidi ya Euro milioni 30 wakati huo ambapo alifunga mabao 23 kwenye msimu wake wa kwanza lakini amekuwa akishuka kwenye orodha ya washambuliaji wa timu hiyo siku hadi siku.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...