facebook likes

Tuesday, July 9, 2013

MARIAH CAREY VIATU VYAMUUMBUA



MUIMBAJI mwenye sauti yenye mvuto nchini Marekani Mariah Carey ajikuta katika wakati mgumu na aibu ya aina yake baada ya viatu virefu maarufu kwa jina la 'high heels' kumdodosha wakati akicheza shoo ya video ya nyimbo inayojulikana kwa jina la 'Beautiful'

Viatu virefu ni moja ya vitu ambavyo muimbaji huyo huvipenda lakini huenda hatotaka tena kuvisikia kutokana na hali iliyompata kudondoshwa na viatu hivyo na kumsababishia maumivu makali na hatimaye kukimbizwa hospitali .


Mtu wakaribu wa mwanamuziki huyo aliiambiwa chanzo kimoja cha habari kuwa ajali hiyo ilitokea wakati wa utengenezaji wa video ya remix ya 'Beautiful' iliyokuwa ikiongozwa na muwewake Nick Canno, ndipo muimbaji huyo alidondoka na kusababisha maumivu ya bega.


Wakati huo huo chanzo kingine kiliuambia mtandao wa New York Post kuwa ajali hiyo ilitokana na viatu virefu alivyokuwa amevaa wakati anacheza video hiyo.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...