SOMA ZAIDI...
Mkataba wa Wenger unamalizika Juni na
wakati anamtambulisha mchezaji mpya ghali wa klabu aliyesajiliwa kwa
Pauni Milioni 42.5, kiungo huyo Mjerumani,kocha huyo wa Arsenal amesema
uamuzi wa kuongeza mkataba wake wa miaka 17 utategemea na matunda
yatakayopatikana na uwekezaji huo mkubwa uliofanywa na klabu.
Alipoulizwa Alhamisi ameanza mazungumzo
ya Mkataba mpya, kocha huyo mwenye umri wa miaka 63 alisema: "Hatuna
haraka. Tupo katika mwezi Septemba na Mkataba wangu unaisha Juni. Kuna
muda mrefu kufika huko. Hakuna haja ya kupanga,"alisema.
Amebeba mustakabali: Arsene Wenger akiwa na mchezaji mpya Mesut Ozil jana katika Mkutano na Waandishi wa Habari
Mazoezi Colney: Kocha Arsene Wenger, akiwa na Mesut Ozil, Per Mertesacker na Msaidizi wake, Steve Bould
Ukame wa mataji: Arsenal ilishinda taji la mwisho mwaka 2005, Kombe la FA Uwanja wa Millennium
"Nimesema mara nyingi, nataka kufanya
vizuri na hii klabu na, mwishowe, nitaketi chini na kufikiria nimefanya
vizuri kiasi gani katika timu. Na hilo litafanya niamua ndio au hapa.
"Moja kati ya maamuzi makuu unayoweza kufanya kuhusu kocha ni amefanya vizuri kiasi gani katika timu,".
Ozil anaamini anaweza akamaliza ukame wa
mataji wa misimu minane na amesema timu yake mpya inaweza kushindani
ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu.
Kifaa: Arsene Wengeramevunja rekodi ya usajili ya klabu kwa kumsaini Mesut Ozil from kutoka Real Madrid
Karibu London: Arsene Wenger akimuongoza Mesut Ozil kwenye Uwanja wa mazoezi wa Colney, London
Sajili sajili sajili: Wenger amekuwa akishinikizwa kusajili
Amepagawa: Wenger na Arsenal hawajashinda taji tangu mwaka 2005, walipotwaa Kombe la FA (chini)
Arsene Wenger akiinua Kombe la lifts theFA
Bais la ushindi: Mashabiki wa Arsenal
wakiwa mitaani Islington mwaka 2004 kuipongeza timu yao katika
maandamano ya kusherehekea ubingwa mjini London
Enzi za raha: Wenger akiwa na taji la Ligi Kuu mwaka 2004 baada ya Arsenal kumaliza msimu bila kufungwa hata mechi moja
Mawili kwa mpigo: Wenger akiwa na taji la Ligi Kuu na Kombe la FA mwaka 2002
Mtu mkubwa: Wenger akiwa na taji la Ligi Kuu ya England aliposhinda mataji mawili kwa mara ya kwanza mwaka 1998
Nani wewe? Wenger alipojiunga na Arsenal mwaka 1998 akiwa hafahamiki wakati huo
No comments:
Post a Comment