
SOMA ZAIDI.....
Mourinho msimu wa 2009/2010 alitamba kwa
kutwaa mataji matatu, na alifanya hivyo ya kumtumia Eto'o nje ya nafasi
yake, akimchezesha pembeni kulia katika washambuliaji watatu
alipomsajili kama mbadala wa Zlatan Ibrahimovic.
Na ni wakati huo Eto'o akifanya kazi na
Mourinho Italia alipoanza kumpenda kocha hujyo Mreno lakini kabla ya
hapo akiwa Barcelona wakati Mreno huyo akiifundisha Chelsea hakutaka
kucheza chini yake.

Marafiki wameungana: Mshambuliaji mpya wa Chelsea, Samuel Eto'o anafurahia kufanya kazi na Jose Mourinho tena
"Kabla ya kukutana naye Inter, tulikuwa
hatufahamiani kila mtu, hivyo uhusiano wetu haukuwa mzuri," Eto'o
aliiambia The Sun. "Niliwahi hadi kusema wakati mmoja kwamba sitakuja
kucheza katika klabu ambayo Jose anaikochi.
"Lakini Mungu anafahamu vizuri. Alitaka kunionyesha kwamba nilikuwa napotoka na leo Jose ni rafiki. Leo ni kocha wangu tena,".
Mkali Eto'o amewasili Chelsea kwa
uhamisho wa Pauni Milioni 7 kutoka Anzhi Makhachkala katika siku ya
mwisho ya ya kufungwa kwa pazia la usajili, baada ya klabu hiyo kufeli
kumsajili mchezaji iliyekuwa ikimtaka sana, Wayne Rooney.

Dole juu: Jose Mourinho hatimaye amempata mshambuliaji aliyemta, Eto'o amewasili
Kuna wakati Mcameroon huyo alipewa hila
ya kuwa matatizo na ubinafasi na hilo lilichangia kuondoka kwake Barca
mwaka 2009, lakini akiwabt Inter, chini ya Mourinho, mambo yaliendelea
kumuendea vizuri.
Eto'o alihusishwa kwa kiasi kikubwa na
kutua Chelsea mwaka 2006, wakati Adriano pia alipokuwa akitakiwa, kabla
ya Andriy Shevchenko kusajiliwa kwa Pauni Milioni 30.

Historia itajirudia? Wawili hao walifanya mambo makubwa walipokuwa Italia na Inter Milan

Mataji matatu: Inter ilitwaa mataji ya
Ligi ya Mabingwa na mawili ya nyumbani msimu wa 2009/2010 wakati
Mourinho akifanya kazi na Eto'o huko
No comments:
Post a Comment