Aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa, Ammy Nando amesema hana majuto yoyote baada ya kuondolewa kwenye shindano hilo.
msikilize hapa:
Nando ambaye aliondolewa wiki iliyopita kwa kuvunja sheria za shindano hilo , leo amefunguka kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha XXL cha Clouds FM.
“I live my life with no regrets,”alisema Nando na kuongeza:
“Sitaki kufikiria matatizo wala nini, kilichotokea ndio kimetokea...
"Najipanga upya ili niendelee na maisha mengine. Vingapi vizuri vimetokea nyuma ?
"Tokea nilipokuwa mtoto mdogo nani alikuwa ananijua? Sasa hivi nipo peace , nashukuru kwamba mmenipokea vizuri.
"Naendelea na maisha, uzuri nimepata platform ya kutengezeza jina langu, kwahiyo naenda hivyo hivyo mpaka huko ntakapofika.
No comments:
Post a Comment