facebook likes

Thursday, August 1, 2013

MSANII WA BONGO FLAVA "DAYNA" ATEMBELEA NA KUWEKA MISHUMAA KWENYE KABULI LA MANGWEA


Dayna akiweka Mshumaa juu ya Kabuli 
 
Mwimbaji wa nyimbo za mafungu ya nyanya, Fimbo ya mapenzi, Nivute kwako na ule unaotamba sasa wa Leo, Dayna Nyange mkali wao, ndani ya mwezi mtukufu, amefanya ziara ya kumkumbumbuka na kutembelea kaburi alilozikwa mwanamuziki mwenzie toka Morogoro, Albert Mangwea
Dayna ameonekana katika kabuli la Mangwea, mwanzoni mwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Akizungumza na mwandishi wa Habari hii mara baada ya tukio, Dayna amesema Albert Mangwea ni mmoja ya wasanii aliokuwa nao karibu sana na alikuwa akimsaidia kwa mambo mengi sna katika mziki

"Unajua Albert Mangwea ni zaidi ya msanii mwenzangu, alikuwa kama ndugu kwangu. Albart alikuwa akinishauli mambo mengi sana juu ya mzikim na hata maisha pia. Hivyo ni wajibu kwangu kumkumbuka mara kwa mara. Pia kitu ambacho hukijui, Ngwea ni mmoja ya wasanii walionisaidia sana hasa kusambaza wimbo wangu huu wa sasa nilioimba na Mr: Blue - Leo. sitamsahau my Brother Ngwea na ndiyo maana ndani ya mwezi mtukufu nimetenga siku ya leo kuja kumtembelea. Pumzika kwa amani japo pengo lako bado lipo'' Amemaliza huku akibubujikwa na machozi.
Dayna akipiga saluti ishara ya kumkubali Marehemu Albert Mangwea
Pumzika kwa amani Ngwea.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...