Gazeti la kila siku la michezo nchini Hispania la AS limeripoti kuwa
Tottenham Hotspurs na Real Madrid zimefikia makubaliano juu ya bei ya
usajili wa Gareth Bale.
Madrid italipa paundi milioni 104 kwa mujibu wa taarifa hiyo na hivyo kumnasa mchezaji huyu ambaye amekuwa akisakwa na mabingwa hao wa zamani wa Spain kwa muda mrefu .
Makubaliano hayo hata hivyo ni ya msingi baina ya klabu hizo na hakuna kitu chochote ambacho kimewekwa rasmi .
Bado klabu hizo mbili hazijakubaliana mfumo wa malipo ya dili hilo na inatarajiwa kuwa Real Madrid itatoa kiasi fulani cha fedha kwa mikupuo kadhaa huku fedha hizo zikiambatana na wachezaji wawili ambao ni Angel Di Maria na Fabio Contreao au mmoja kati ya wachezaji hao . Andre Villas Boas ametajwa kuvutiwa na beki uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani Fabio Contreao ambaye anamfahamu tangu nchini Ureno .
Wakati hayo yakiendelea Spurs wamekamilisha usajili wa mshambuliaji Roberto Soldado toka klabu ya Valencia.
Soldado amesajiliwa kwa paundi milioni 26 na taratibu za usajili wake zitakamilika baada ya mchezaji huyo kufanyiwa vipimo vya afya .

No comments:
Post a Comment