facebook likes

Friday, August 30, 2013

ARSENAL NA BARCA KATIKA KUNDI LA KIFO LIGI YA MABINGWA

 MABINGWA mara saba wa Ulaya, AC Milan, waliotolewa na Barcelona katika Ligi ya Mabingwa misimu miwili iliyopita, wamepangwa kundi moja na vigogo hao wa Katalunya katika hatua ya makundi msimu huu baada ya droo iliyopangwa jana.
SOMA ZAIDI..........

Arsenal ambayo kocha wake Arsene Wenger anapambana kusajili jina kubwa kabla ya pazia kufungwa, imepangwa Kundi F pamoja na Marseille ya Ufaransa, Borussia Dortmund ya Ujerumani na Napoli ya Italia.
Mabingwa mara tisa, Real Madrid wamepangwa kundi moja na Juventus, B ambalo pia lina timu za Galatasaray and FC Copenhagen.

Mabingwa watetezi, Bayern Munich wamepangwa na CSKA Moscow, Manchester City na mabingwa wa Czech, Viktoria Plzen Kundi D, ambayo inawapa njia nyeupe ya kufuzu.
Chelsea, mabingwa wa misimu miwili iliyopita, wamepangwa na Schalke 04, FC Basle na Steaua Bucharest Kundi E, timu mbili ambazo ilizifunga kuelekea kutwaa taji la Europa League msimu uliopita.
Mabingwa mara tatu wa taji hilo, Manchester United imepangwa na Shakhtar Donetsk, Bayer Leverkusen na Real Sociedad katika Kundi A.
AC Milan na Barcelona wamekutana mara sita katika misimu miwili iliyopita na Wakalunya wameng’ara dhidi ya Wataliano.

KUNDI A

Manchester United
Shakhtar Donetsk
Bayer Leverkusen
Real Sociedad

KUNDI B

Real Madrid
Juventus
Galatasaray
FC Copenhagen

KUNDI C

Benfica
Paris Saint-Germain
Olympiakos
Anderlecht

KUNDI D

Bayern Munich
CSKA Moscow
Manchester City
Viktoria Plzen

KUNDI E

Chelsea
Schalke
Basle
Steaua Bucharest

KUNDI F

Arsenal
Marseille
Borussia Dortmund
Napoli

KUNDI G

Porto
Atletico Madrid
Zenit St Petersburg
Austria Vienna

KUNDI H

Barcelona
AC Milan
Ajax
Celtic
87 matches.jpg
Timu ya Serie A ilifungwa mabao 4-2 jumla katika hatua ya 16 Bora mwaka jana na 3-1 jumla katika Robo Fainali misimu miwili iliyopita, wakati timu hizo zilipokutana pia kwenye hatua ya makundi.
Timu hizo mbili zimepangwa katika Kundi H, sambamba na mabingwa mara nne Ajax Amsterdam na mabingwa wa 1967, Celtic, ambao walikutana na Barcelona katika hatua ya makundi msimu uliopita na kupata ushindi wa kukumbukwa wa nyumbani.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...