facebook likes

Friday, August 30, 2013

HUYU NDO MSANII WA FILAMU ALIYE NUSURIKA KIFO


MSANII wa filamu za Kibongo, Prisca Tadei hivi karibuni alinusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya ya pikipiki wakati alipokuwa akielekea ‘location’ kushuti. 
SOMA ZAIDI........Ajali hiyo ilitokea wiki iliyopita maeneo ya Mbagala, jijini Dar ambapo Prisca aliumia 
vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya pikipiki aliyokuwa amepanda kugongwa na gari ambapo alikimbizwa Hospitali ya Mnazi Mmoja na kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Akichonga na paparazi wetu, mkurugenzi wa kikundi anachofanyanacho kazi cha Kalunde Entertainment, Mariamu Athuman ‘Kalunde’ alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa msanii wake huyo mpaka sasa anapumua na anaonesha matumaini kwani ilikuwa ajali mbaya.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...