facebook likes

Thursday, June 27, 2013

Wakati huu ambapo mengi yanasemwa kuhusiana na Afya ya Nelson Mandela, Hiki ndicho kinachoendelea Afrika Kusini kwa sasa












Kwa Mujibu wa BBC, Mandela anaendelea kupokea matibabu hospitalini, na Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana mjini Cape Town, Afrika Kusini, Thabo Makgoba, amejitolea kufanya maombi kwa niaba ya rais mstaafu Nelson Mandela ambaye anaugua sana hospitalini. Kasisi huyo anamuombea Mandela aweze kupata nafuu na amewataka wananchi kumshukuru kwa yote aliyowafanyia.
Maombi hayo yalitolewa baada ya Askofuu huyo kumtembelea Mandela hospitalini ambako kiongozi huiyo wa zamani amekuwa akilazwa kwa wiki mbili na nusu zilizopita baada ya kuugua mapafu.

Habari inayoleta wasiwasi mkubwa juu ya Mustakabali wa Afya ya Mandela ni hatua ya wajukuu wa rais huyo wa zamani wa Afrika kusini wanakutana nyumbani kwake kijijini katika mkoa wa Eastern Cape province, ambako viongozi wa kitamaduni wamealikwa kujadili mambo ambayo bado hayajafahamika kwa uhakika, wakati pia ndugu zake wengine wamekutana nyumbani kwake huko Kunu, huku hali yake ya afya ikizidi kudorora hospitalini, Pretoria.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...