KIJANA wa Kitanzania Hamisi Kondo ameibuka mshindi wa dunia katika mashindano ya kuruka kamba yaliyofanyika nchini Marekani Julia 5 hadi Julai 13 mwaka huu. Mashindano hayo yalihusisha nchi 14 zikiwa na wachezaji 480, huku Bara la Afrika likiwakilishwa na Tanzania, Kenya na Afrika ya Kusini ambapo kijana Hamisi mwenye umri wa miaka 14 Mtanzania aliweza kujinyakulia ushindi huo.Kijana huyo ambaye ni yatima aliyelelewa na kituo cha kulelea watoto yatima cha Dogodogo Center kilichopo jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya mchezo wa kuruka kamba kituoni hapo na baadae kupata ufadhili kutoka kwa Bwana na Bibi Amy Canady nchini Marekani ambako aliweza kusoma na kuendeleza kipaji chake.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Hamisi amezungumzia mafanikio yake na kuwaasa vijana wenzake kutokata tamaa ya maisha kwa kuwa na juhudi ya kupambana ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
“Nawaomba watoto wa mtaani na yatima kutokata tamaa ya maisha kwani hata mimi nilikuwa kama wao na nimeweza kufanya juhudi na kufanikiwa,” alisema Hamisi.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda aliwaomba vijana kutong’ang’ania michezo mikubwa kama mpira wa miguu kwani kuna michezo midogo midogo ambayo wanaweza kucheza na kufanikiwa kama ilivyo kuwa kwa Hamisi.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda aliwaomba vijana kutong’ang’ania michezo mikubwa kama mpira wa miguu kwani kuna michezo midogo midogo ambayo wanaweza kucheza na kufanikiwa kama ilivyo kuwa kwa Hamisi.
Pia Mwenyekiti wa Kituo cha Kufundisha Michezo Tanzania (TSTC), Bw. Dennis Makoi ambaye alishirikiana na kituo cha dogodogo kumtafutia ufadhili Hamisi nchini Marekani, ametoa shukrani zake za dhati kwa familia ya Bw. na Bi. Amy Canady wa huko Marekana kwa ufadhili na kusaidia kufanikisha ushindi huo. Hivi sasa Hamisi anaendelea na masomo nchini Marekani.
Via: thehabari
No comments:
Post a Comment