facebook likes

Friday, August 2, 2013

BERLUSCONI ACHEMKA BAADA YA KORTI KUDUMISHA KIFUNGO

Silvio Berlusconi
Bw Silvio Berlusconi. Pichani.
Waziri Mkuu wa zamani Silvio Berlusconi amepeperusha ujumbe wa hasira wa video baada ya mahakama ya juu zaidi ya Italia kuthibitisha kifungo alichopewa kwa makosa ya ulaghai wa ushuru.
WAZIRI Mkuu wa zamani Silvio Berlusconi amepeperusha ujumbe wa hasira wa video baada ya mahakama ya juu zaidi ya Italia kuthibitisha kifungo alichopewa kwa makosa ya ulaghai wa ushuru.
Berlusconi alisema ni mwathiriwa asiye na hatia wa “msururu wa shutuma na mashtaka ya ajabu yasiyo na uhalisi wowote.”
Mahakama hiyo pia iliagiza uchunguzi zaidi wa mahakama iwapo anafaa kupigwa marufuku kushikilia wadhifa wowote wa umma.
Berlusconi, 76, yawezekana hataenda jela kutokana na umri wake.
Huku akitarajiwa kutekeleza adhabu yake kwa kifungo cha nyumbani, ana chaguo la kutumikia jamii badala yake, huku makataa ya kuwasilisha ombi hilo yakitarajiwa kuwa Oktoba.
Uamuzi wa mahakama hiyo ya Rome’s Court of Cassation, ambayo hawezi kukata rufaa dhidi yake, ulikujia baada ya siku tatu za kusikilizwa kwa kesi hiyo. Berlusconi hakuwa kortini.
Katika ujumbe wa dakika tisa wa video, Berlusconi alikashifu uamuzi huo kama “usio na msingi wowote, na unaoninyima haki yangu ya uhuru na kisiasa.”
“Hakuna anayeweza kuelewa shambulio hili la kunivuruga kabisa kufuatia msururu wa shutuma na mashtaka ambayo hayana uhalisi wowote,” alisema.
Anaelezea kesi hizo zaidi ya 50 alizokabiliwa nazo kama “dhuluma halisi ya mahakama ambayo haijaonekana kwingine katika ulimwengu wa sasa.”
Mgawanyiko
Alishutumu utendakazi wa idara ya mahakama ya nchi hiyo, akisema: “Je, hii ndiyo Italia tunayotaka? Je, hii ndiyo Italia tunayopenda? La hasha!”
Kesi ya kifungo alichopewa inahusu dili ambazo shirika lake la Mediaset lilifanya ili kununua haki ya kupeperusha filamu za Amerika kwenye televisheni.
Adhabu hiyo iliyotolewa Alhamisi ndiyo ya kwanza hakika dhidi ya mfanyabiashara huyo bilionea baada ya miongo kadha ya kuandamwa na mashtaka ya uhalifu.
Aidha, ni hatua ambayo pia imeyumbisha siasa za mgawanyiko nchini Italia.
Waziri mkuu Enrico Letta aliomba kuwe na utulivu “kwa manufaa ya taifa” huku kukiwa na hofu kuwa uamuzi huo wa aina yake ungesababisha mivutano katika serikali ya muungano inayojumuisha chama cha Berlusconi cha People of Freedom.
Mawaziri wa Berlusconi walisema wanatafuta uwezekano wa kukata rufaa katika Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...