Duru za ngazi za juu katika chama cha ZANU-PF nchini Zimbabwe zimedai kuwa Rais Robert Mugabe amemshinda Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai wa chama cha MDC katika uchaguzi wa rais na bunge uliofanyka jana nchini humo.
Afisa mwandamizi wa ZANU-PF ambaye hakutaka kutajwa amenukuliwa na Reuters akisema: ‘Tumeshinda uchaguzi huu. Tumekizika chama cha MDC. Hatukuwa na shaka yoyote kuhusu ushindi wetu.’
Kutangaza matokeo ya mapema nchini Zimbabwe ni kinyume cha sheria na polisi wamesema watamkamata yeyote atakaye tangaza matokeo yasiyo rasmi.
Punde baada ya ZANU-PF kutoa tangazo hilo, chama cha MDC cha Tsvangirai kimesema kumekuwepo na ‘wizi mkubwa wa kura’ katika uchaguzi. Afisa mwandamizi wa MDC ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema hawatakubali matokeo ya uchaguzi na kwamba chama hicho kitaitisha kikao cha dharura baadaye leo.
Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe Rita Makarau amesema anaamini uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kwamba idadi kubwa ya wapiga kura milioni 6.5 walijitokeza. Aidha waangalizi wa Umoja wa Afrika katika ripoti ya awali wamesema uchaguzi wa Zimbabwe ulikuwa wa ‘amani, wenye nidhamu, huru na wa haki.’

No comments:
Post a Comment