Dar es Salaam.Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Kim Poulsen amesema kitendo cha kipa Juma Kaseja kujiunga na klabu ya FC Lupopo, DR Congo kitafungua milango ya mafanikio ya soka la Tanzania.
FC Lupopo kupitia kwa meneja wake Balanga Ismail juzi ilitangaza kuridhia kumsajili Kaseja kwa mkataba wa miaka mitatu ukiwa na thamani ya Dola za Kimarekani elfu 30.
Akizungumza na Mwananchi jana, Kim alisema ni faraja kwake kuona idadi ya wachezaji wanaokwenda kucheza soka nje ya nchi inaongezea siku baada ya siku, kitu ambacho ni ishara ya mafanikio kwa soka la Tanzania.
“Nimepata taarifa ya Kaseja kutakiwa FC Lupopo, hakika ni jambo la kuleta matumaini katika soka la Tanzania,”alisema Kim na kuongeza:
“Mimi siifahamu vizuri, lakini nimeambiwa ni moja kati ya klabu kubwa kule, ni matumaini yangu uzoefu atakaoupata utaisaidia pia nchi yake,”alisema Kim.
Alisema, anatarajia baada ya miaka michache ijayo Tanzania itakuwa na idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, hivyo kumpa wigo mpana wa kuteua wachezaji kwa ajili ya kikosi cha Timu ya Taifa.
“Kama hivi sasa kuna Kapombe (Shomari) amekwenda Uholanzi kufanya majaribio kama akifanikiwa ni jambo zuri, ni matumaini yangu miaka michache ijayo watakuwa wengi zaidi na hivyo kufanya kazi ya kuteua wachezaji wa kuunda timu ya taifa kuwa rahisi,”alisema Kim.
Kaseja ataungana na nyota wengine wawili wa Tanzania wanaokipiga Ligi Kuu ya DR Congo ambao ni Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaoichezea klabu ya TP Mazembe.

No comments:
Post a Comment