facebook likes

Friday, August 2, 2013

MKE WA DR. SLAA AZUA TIMBWILI MAHAKAMANI

JOSEPHINE Mushumbusi, mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa,jana alisababisha vicheko mahakamani baada ya kushindwa kumtambua mshtakiwa anayedaiwa kumpora maeneo ya SUMA JKT.

 

Josephine alimuacha mshtakiwam katika kesi yake na kumtambulisha 
mshitakiwa wa kesi nyingine kuwa ni miongoni wa watuhumiwa waliomvamia.

Hayo yalitokea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa alipokuwa akitoa ushahidi kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali Leonard Chalo.

Washitakiwa katika kesi hiyo ambao wanakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha ni Getisi Mturi, Gake Mwita, Salum Mpanda na Charles Chasens.

Mturi na wenzake wanadaiwa Julai 13, 2011, eneo la Suma JKT makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi, walimvamia Josephine na kumpora vitu mbalimbali na kabla ya kufanya uhalifu huo walimtishia kwa silaha.

Josephine alidai Julai 13 mwaka 2011, aliingia ofisini kwake katika jengo la Mawasiliano Tower saa 2.00 asubuhi na kutoka saa 11.00 jioni kwenda nyumbani kwake eneo la Boko akiendesha gari aina ya Toyota Harrier.

Alidai akiwa eneo la tukio katika foleni alimwona mtu akipita mkono wa kushoto huku akimuangalia kwa kutumia kioo cha pembezoni na ghafla alimuona akivunja kioo cha gari lake.

Josephine aliidai alipoanza kuvunja dirisha alitahamaki lakini alisikia risasi hivyo aliamua kutafuta jinsi ya kujiokoa kwa kutoa gari eneo hilo na kwenda katika geti lililopo karibu na Suma JKT.

“Nilifanikiwa kuona sura ya mtu aliyenivamia kwa kuwa tulisimama wote kwa takribani dakika nane,”alidai Josephine.

Josephine alidai katika tukio hilo anakumbuka kulikuwa na watu si chini ya sita na walimwibia vitu mbalimbali. Kesi hiyo imepangwa kuendelea kusikilizwa Agosti 7 mwaka huu

source:thechoice
http://www.thechoicetz.com/2013/08/mke-wa-dr-slaa-azua-timbwili-mahakamani.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+blogspot%2FGDSbw+%28TheCHOICE%29

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...