facebook likes

Friday, August 2, 2013

Soma maswali na majibu aliyoyatoa Nando kwenye interview yake ya kwanza toka atoke BBA.



2
Ile interview ya mshiriki wa Big brother the Chase Ammynando akiwa kwenye XXL  ya Clouds fm ndio hii, kwa kuelewa kwamba kuna walioshindwa kusikiliza Radio na kuona video za interview, hii time nimeitumia kuandika maswali na majibu ya yote aliyoyazungumza Nando.
Miongoni mwa aliyozungumzia Nando ni pamoja na kuingia na kisu kwenye party, maisha yake halisi na mambo mengine mengi ambapo aliambatana na Barbara Kambogi meneja uhusiano wa MultiChoice Tanzania.
ADAM MCHOMVU: Nando do you speak Swahili ?
NANDO: Mimi ni mtoto wa kitaa mzee kwetu ni Mikocheni napiga kiswahili kamakawa.
B12: Mimi nilijua unaongea sana kiswahili siku ambayo kulikuwa kuna party ndani ya jumba la big brother na ukawa unaongea na Feza ukamwambia, “Feza eh, mtoto Selly nishamalizana naye nipe Pokello” Feza ikabidi amvute Diamond house huku umalizane naye.
NANDO: Unajua tulishaonywa kama mara mbili tatu hivi tusiongee kiswahili sema mswahili si utamjua tu.
B12: Sema mlikuwa mnaelewana sana na mwanadada Annabel kutoka Kenya ukiachana na mshkaji wako Bimp, kwanini yani?
NANDO: Annabel yule mwanamke ana akili sana, anakimbilia Master sasa hivi, mchangamfu, anacheza, chakula ananipikia yeye, yani kila kitu tulikuwa tunafanya mimi na yeye…. kwanini nisimpinde mtu kama yeye ambaye ananirahisishia maisha mwanangu. ADAM MCHOMVU: Wakati upo Big brother ulikuwa unamiss kitu gani huku nje?
NANDO: Nilikuwa namiss sana internet aisee, yani nilitaka hadi nitengeneze kibox cha sabuni niandike namba nicheze nacho aisee.
ADAM MCHOMVU: Oky, sasa hivi umetoka kwenye lile jumba, ni nini unamiss?
NANDO: Kusema ukweli mi nilikua nishachoka mle ndani aisee sikutanii mwanangu, sema imetokea bahati mbaya sio kama nimekusudia, kila binadamu ana sehemu mbili, nzuri na mbaya… siku ikiwa mbaya basi ukiharibu tu ndiyo hivyo kama ilivyotokea.
2
DJ FETTY : Nando ulikuwa ni mshiriki ambaye unakubalika na karibia Afrika nzima kutokana na life style yako mle ndani, Japokuwa ulitolewa lakini tulikuwa tunasoma sms za watu wakiku-support, sasa maisha yale ndani ya jumba ndiyo yako halisi au ilikuwa mipango yako tu katika game?
NANDO: Unajua mimi mwanangu nimeingia kwenye jumba lile na kiatu pea moja tu, hichohicho nimechezea mpira yani nimeenda kama mimi, sijaenda eti sijui ninyoe nywele sijui nifanye hivi… mimi nimeenda nikawambia sikilizeni, sivai hizi bukta zenu wala nini….. walininunulia moja ya njano lakini sijaivaa hadi leo sema wanakuchukua wanaku-take care lakini nilibaki kuwa mimi.
ADAM MCHOMVU: Game ilikuwa ni kitu gani pale kwenye nyumba?
NANDO: Mimi sikucheza game pale kwa sababu hata niliwaambia mimi sitacheza game, mambo ya kusengenyana, kuchukiana mimi hapana, niliwaambia nitaishi maisha nyangu, ukiniambia ukweli nakwambia ukweli usiponiambia na mimi sikwambii.
B12: So umetoka kwenye Big brother Africa lakini kuna Watanzania kibao hawajui nini kili happen hadi ukatoka?
NANDO: Unajua yule jamaa tangu tumeingia siku ya kwanza alikuwa anatoa maswala ya kizushi kizushi halafu mimi nabaki namuangalia tu.
DJ FETTY: Jamaa mwenyewe unayemzungumzia ni Elikeem kutoka Ghana?
NANDO: Eh huyohuyo naskia siku hizi wanaandamana lakini fresh watanzania wako hapa bwana na mimi ni mtanzania,  kosa nililofanya lilikuwa ni pale mtu unapokuwa na dukuduku unatakiwa ulitoe lakini ukilijaza na kulijaza ukitoa linakuwa bomu, huyu jamaa bwana alichukua barafu alafu anarusha kwenye dance floor, sasa mtu utarushaje ice cubes kwenye dance floor then ndiyo huyohuyo jamaa Wanawake wanamuongelea kila kitu.
‘Sasa unamtetea kwamba huyu mwanangu kisa mvulana lakini basi hajaskia halafu kwenye topic ya kijinga sana pombe tu, ikabidi nimwambie yote, kila mtu anastaili yake… kuna ile ukiweka dukuduku likijaa tu haliishi vizuri’ – Nando
9
ADAM MCHOMVU: Oky labda ni bahati mbaya hiyo, mfano ungeshinda ule mkwanja ulikuwa na mpango gani?
NANDO: Tangu nimefika Big brother imepigwa video moja tu ya kitanzania ambayo ilikuwa ni ya Feza, Tanzania ndiyo tunakuwa kila siku sasa kuna ile kitu ya Wanigeria, West africa sana…  hata tukiwa mle ndani hakukupigwa hata wimbo mmoja wa Tanzania kwenye zile playback, sana sana ngoma za Kenya kama Wyre na ile ngoma ya nchi ya kitu kidogo…. So mimi nitaka tutoboe kiubishibishi sana hadi level zile, sikutanii kama ningeshinda ningekuja ku-invest kwenye Entertainment.
DJ FETTY: Katika historia yako umetoka US umekuja hapa kwa kuomba washkaji pesa ya ticket, tumeona kwa asilimia 90 umeweza baada ya kuingia mle ndani, what is the feeling baada ya ndoto zako kuishia njiani wakati umetoka Marekani hadi Dar kwa ajili ya hiki kitu.
NANDO: Bonge la swali, yani mimi ni mtu ambaye naishi maisha yangu with no regret, kila kilichotokea wacha kipite na maisha yanaendelea mbele, mangapi yametokea huko tangu niko mdogo hakuna anayejua labda Barbara ambaye aliniona kwenye audition wengine wote wamenisikia tu, mimi ni mtu wa vyovyote vile ninachoshukuru nimepokelewa vizuri kuanzia airport japokuwa wengine wanaongea tofauti lakini ndiyo hivyo tena, nimeingia mle nimepata platform ya kutengeneza jina kwa hiyo mambo mengine yanaendelea.
ADAM MCHOMVU: Hadi hivi sasa karibia Africa nzima inakujua, ni kitu gani unataka kukifanya kama Nando.
NANDO: Mimi ni mtu wa suprise sana kama ulivyoona kwenye Big brother nimeingia kwa suprise hakuna aliyejua, unatakiwa uumize kichwa juu ya kipi cha kufanya na mimi nahitaji huo muda wa kuchil na kuumiza kichwa nifanye nini.
ADAM MCHOMVU: Music labda,movie au soka?
NANDO: Kila kitu mwanangu lakini soka siwezi tena kama unavyoona nilivyoumia.
1
B12: Ilikuaje hiyo miguu?
NANDO: Hapa unajua nilitoroka shule tukawa tunapiga game pale shule ya ushindi, kipa akanirukia miguu yote miwili bwana, nikaenda nikafanyiwa upasuaji naamka asubihi miguu yote haifanyi kazi nikaenda kufanya majaribio ya mashule makubwa sana nikaumia tena, so ni kama haikupangwa mimi kwenye soka hivi.
B12: Bado tupo na Nando kwenye XXL tunataka atuambie nani anahisi atakuwa mshindi wa big brother the chase lakini hivi sasa itabidi atuambie ngoma gani anapenda kuisikiliza tuigonge hapa.
NANDO: Weka ngoma ya dada yangu Feza aisee, tumpigieni kura ashinde angalau aje anipe kama dola elfu kumi hivi tushaongea naye.
B12 : Tupo na meneja uhusiano wa Dstv Barbara, embu tuambie jinsi utaratibu wa kumpigia kura Feza.
BARBARA: Hii wiki ni kali sana kwetu tunasikitika kuona Nando amerudi lakini ndio hivyo kama binadamu unajirudi unaendelea na maisha lakini mshiriki mmoja ambaye ni Feza bado yupo BBA na yupo kwenye enviction wiki hii, dola laki tatu za kimarekani ni nyingi jamani tupige kura kumsave Feza ikiwa zimebaki wiki tatu tu.
Chakufanya ni kupiga kura kwa njia mbili moja ni kutuma neno Vote Feza kwenda 15456 kwenye mitandao yote pia kwa kupitia www.bigbrotherafrica.com ambapo ukipiga kura hapa unaweza kushinda zawadi mbalimbali.
11
B12: Kwa watu ambao wanataka kushiriki mwakani kwenye Big brother Africa, sifa ya kwanza ni ipi?
BARBARA: Kwanza pale tunavyotaka washiriki kwenda Big brother huwa tunatangaza rasmi kama tunataka washiriki, kigezo cha kwanza ni umri, mshiriki lazima awe na miaka 21 kwasababu mtu mwenye umri huu anaweza kufanya maamuzi mwenyewe, pili lazima awe na passport kwa ajili ya kusafiria, tatu lazima awe anajua lugha ya kiingereza kwa ajili ya kuwasiliana ndani ya jumba la Big brother.
DJ FETTY: Kuna watu wengi walifika kwenye audition wenye hizo sifa, lakini kipi kilikua special kwa Nando na sio wengine?
BARBARA: Kwanza kabisa wakati wa audition tunakuwa na Endemol ambao ndio main producers wa show ya Big brother, wao ndio wahusika wakuu kwenye audition sisi ni kama wenyeji tu.
DJ FETTY: Nando siku ya kwanza kabisa ulivyoingia Big brother ulimwambia Big we need more girls, dizain haukuwaona wa mle ndani nini?
NANDO: Mle ndani kuna hasara tupu yani hakuna kumwamini mtu kwasababu wengi wanaongea lakini action ndogo, Wanawake wenyewe walikuwa wanalalamika hasa kwenye diamond house ambako kulikuwa na young star sana sana yani kama yule Dillish ndiyo hakuna kitu kabisa.
B12: Lakini dezayn kama ulikoma naye sana mtoto Dillish yule wa Namibia.
NANDO: Si unajua yeye mbishi kama mimi, siku nyingine ananinunia lakini kesho yake kama kawaida.
Dillish
B12: So unafikiri nani atashinda kwenye Big brother.
NANDO: Kama sio brother wangu Bimp kuna Beverly na Cleo, Angelo na Elikeem sina uhakika ila wanaweza
B12: Mahusiano yako na Bimp yali-click vibaya mno zaidi ya mtu yoyote mle ndani unafikiri ni kwasababu gani?
NANDO: Bimp kwanza anafanana sana na kaka yangu, amenisaidia sana hadi siku ya mwisho alikuja kuniuliza kuhusu ule mkasi.
DJ FETTY: Kwanini uliingia na kisu kwenye party?
NANDO: Tangu niko mdogo nimekuwa naomba toys za mpira, kisu, bunduki lakini sio kwamba nimetumia hapana, napenda tu hata nikizeeka nitakuwa na visu.
DJFETTY: Au ndiyo ile kwamba kama hauna nguvu hata uwe na mkwara?
NANDO:Hapana mimi natembea na watu kama 20 niogope nini.
10
DJ FETTY:Wakati Big brother anakuondoa alishakupa warning tatu moja ni kuwa na kisu kwenye party nyingine kushika mkasi ukiwa unagombana na Elikem na kitu kingine sijui ilikuwa ni hasira pale ambapo uliposema alistahili kufa.
NANDO: Yah, that day wote tulikuwa na warning mbili mbili ila baada ya ku-provoke na ndio mimi akaniita ya tatu ndani mle na kunambia kuhusu kumtishia amani.
DJ FETTY: Lakini point yangu ni kwamba Bimp aliendelea kuwa mashkaji wako na alimnominate Elikem na kusema hayuko real na kusema Cleo ndio alichochea ule ugomvi
NANDO:Cleo ni mfuata mkumbo na Elikem anatabia za kitoto sana, mtu wa kuongea ongea sana… tabia aliyokuwa nayo sasa hivi yale mambo mimi nimeyafanya zamani sana nikiwa na miaka 16 au 17 huko, utakuta watu wote wapo kimya lakini yeye anaongea, sasa Cleo kuna siku alifanya hivyo Bimp akakasirika kwasababu walimshtumu kitu flani.
ADAM MCHOMVU: Kitu gani cha mwisho cha kuwambia mafans wako?
NANDO: Nawashukuru sana, mimi mwanenu mtoto wenu na ni mtanzania halisi nimekulia kule Mikocheni ndanindani kule, nimeumwa malaria sana kule, cheza sana kwemye vumbi.
8


source:millardayo

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...