MAAJABU:ROCK RESTAURANT MGAHAWA ULIOJENGWA JUU YA MWAMBA BAHARINI VISIWANI ZANZIBAR..TAZAMA MAPICHA HAPA
Duniani
kuna maajabu mengi,kati ya maajabu hayo ni huu mgahawa uitwao Rock
uliopo visiwani Zanzibar uliojengwa juu ya mwamba mkubwa katika bahari
ya Hindi. ANGALIA PICHA ZAIDI.........
Mgahawa
huo ulifunguliwa rasmi mwaka jana na kuna viti 45 ambapo wateja
huchukuliwa na boti maalum kutoka pwani hadi kupata huduma katika
mgahawa huo ili wasikanyage maji wakati wakiingia kwenye mgahawa huo.
Chakula kinachopatikana muda wote katika mgahawa huo ni samaki pekee kutoka baharini na vinywaji.
Wafanyakazi wa The Rock
The
Rock umetajwa kuwa ni mgahawa wa ajabu katika Afrika Mashariki na watu
wengi wakiwemo watalii hupenda kwenda kutokana na habari zake kuenenea
kwa kasi na wengi hupendelea kupata hewa safi ya baharini na kuona jinsi
kilivyokuwa ndani.
Rock,
ambayo ilifunguliwa mwaka jana, inaweza kufikiwa kwa miguu, lakini pia
kuna usafiri wa mashua wa kuwasafirisha wateja kutoka pwani hadi kwenye
mgahawa huo.
No comments:
Post a Comment