Uamuzi
wa hivi karibuni wa kampuni ya Facebook wa kulegeza sera ya kutoingilia
uhuru wa wateja ulisababisha gumzo lakini katika taarifa nyingine,
imeripotiwa kwamba aliyegundua kampuni hiyo ambaye pia ndio bosi wake,
Mark Zuckerberg ametumia dola za Kimarekani milioni 30 kununua nyumba
nne za jirani kwake kulinda uhuru wake.
Bilionea
huyo mwenye miaka 29 mwenye jumba lake la kifahari kwenye eneo la Palo
Alto, amelipia dau kubwa zaidi kununua nyumba hizo jirani yake ambako
aliyokuwa anaishi tokea mwaka 2011.
Pamoja
na kwamba ana uwezo wa kununua nyumba hizo kwa ajili ya kupanua nyumba
yake, inasemekana kwamba uamuzi wake umetokana na mjenzi mmoja kutaka
kununua eneo la jirani na nyumbani kwake na kulitangaza kwa kutumia jina
lake.
kwa
mujibu wa vyanzo vya habari, Zuckerberg anampango wa kuzikodisha kwa
wapangaji wa sasa ili baadae waweze kuzinunua moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment