facebook likes

Monday, September 9, 2013

KOMBE LA DUNIA-AFRIKA: CAMEROUN YANYAKUA NAFASI YA MWISHO!!

>>10 ZA RAUNDI YA MWISHO YA MTOANO ZAKAMILIKA!!
>>DROO KUPANGWA SEPTEMBA 16!!
SOMA ZAIDI........
Cameroon imetwaa nafasi ya mwisho ya Timu 10 ambazo ni Washindi wa Makundi 10 ambao watacheza Raundi ya Mwisho ya Mtoano ili kupata Timu 5 za Afrika zitakazocheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwakani baada ya leo huko Stade Omnisports, Jijini Yaonde kuifunga Libya Bao 1-0 katika Mechi ya mwisho ya Kundi I.
Bao la ushindi la Cameroun lilifungwa kwa kichwa na Aurelien Chedjou katika Dakika ya 42.
Kwenye Kundi hili Cameroun walinufaika na uamuzi wa FIFA wa kuwapokonya Togo Pointi 3 na kuwapa wao baada ya Togo kumchezesha Alexis Romao, ambae alipaswa kufungiwa kwa kuwa alikuwa na Kadi, katika Mechi ya Juni 9 ambayo Togo iliifunga Cameroun 2-0.
Uamuzi huo wa FIFA uliwafanya leo Cameroun waingie kwenye Mechi hii ya mwisho wakihitaji Sare tu.
VIKOSI:
CAMEROUN: Charles ITANDJE, Nicolas NKOULOU, Dany NOUNKEU, Alexandre SONG [Landry NGUEMO 87'], Samuel ETOO [Jacques ZOUA 60'], Jean MAKOUN [Stephane MBIA 20], Gaetan BONG, Eric CHOUPO MOTING, Aurelien CHEDJOU, Enoh EYONG, Joel MATIP
LIBYA: Mohamed NASHNUSH, Younes SHIBANI, Marwan AHMED, Ahmed OSMAN, Mohamed ALMAGRABI, Osama ABDUSALAM, Ali SALAMA, Ahmed ELTRBI, Abobakari EL SWANEI [Omar ABDELSALAM 60'], Faisal SALEH [Gamal MOHAMED 45'], Eamon ZAYED [Mohamed GHANUDI 73']
++++++++++++++++++++++++++
ZILIZOINGIA RAUNDI YA MWISHO YA MTOANO YA TIMU 10:
-Ethiopia [KUNDI A]
-Cape Verde [KUNDI B]
-Ivory Coast [KUNDI C]
-Ghana [KUNDI D]
-Burkina Faso [KUNDI E]
-Nigeria [KUNDI F]
-Egypt [KUNDI G]
-Algeria [KUNDI H]
-Cameroun [KUNDI I]
-Senegal [KUNDI J]
***KATI YA 10 NI 5 TU ZITAENDA BRAZIL
++++++++++++++++++++++++++
Droo Septemba 16
FIFA imethibitisha kuwa Droo ya kupanga Mechi 5 za Raundi ya Mwisho ya Mtoano itakayotoa Timu 5 za Afrika zitakazoenda Fainali ya Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka 2014 itafanyika Mjini Cairo, Misri hapo Septemba 16.
Droo hiyo itahusisha Timu 10 zilizomaliza Washindi wa Kwanza wa Makundi 10 ya Raundi ya Pili ambapo zitapangwa Mechi 5 zitakazochezwa Nyumbani na Ugenini kupata Timu 5 zitakazoiwakilisha Afrika huko Brazil.
Mfumo wa Droo hiyo utazingatia kuzibagua Timu hizo 10 na kuziweka kwenye Vyungu viwili tofauti huku Chungu Na 1 kikiwa na Timu 5 ambazo ziko juu kwenye Lisiti ya FIFA ya Ubora Duniani na 5 za Chungu Na 2 ni zile zilizokuwa chini kwenye Listi hiyo ya FIFA ili Timu ya Bora zisikutanishwe wakati Timu za Chungu Na 1 zikipangiwa kucheza na Timu za Chungu Na 2.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...