facebook likes

Monday, September 9, 2013

QUEEN DARLEEN ATOA SABABU KWANINI MPAKA LEO HAJAFANYA WIMBO NA MDOGO WAKE DIAMOND


Pamoja na kwamba kaka yake, Diamond kuwa msanii mkubwa na mwenye mafanikio, Queen Darleen hafikirii kufanya collabo naye hivi karibuni.
SOMA ZAIDI........
Akizungumza, msanii huyo wa siku nyingi amesema hana haraka kwakuwa Diamond anamuona kila siku na bado anataka akue zaidi ya hapo.


“Nafikiri mimi namchukulia ni mdogo wangu na ninaamini kwamba yupo na ninampa nafasi aendelee kufanya kazi nzuri zaidi. Kwasababu nikifanya naye sasa hivi ntakuwa nimepoteza maana nzima ya udugu,” alisema Queen.

“Kila siku akija namwambia bado, bado kufanya nyimbo na mimi. Najua kwamba yupo juu zaidi yangu lakini still kwangu yupo chini sababu mimi ni dada yake na ananiheshimu na mimi namheshimu.”

Amesema kila kitu anachofanya Diamond humshirikisha dada yake huyo na yeye amekuwa mshauri wake mzuri.

“Hawezi kutoa nyimbo redioni bila kunisikilizisha mimi, si yeye, si Dully Sykes, si Ali Kiba, wote wako hivyo.”

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...