facebook likes

Monday, September 9, 2013

MADIWANI WATAKA SHERIA YA KUWALAZIMISHA WANAUME KWENDA KLINIKI ITUNGWE


BAADHI ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Itilima mkoani Simiyu wameomba itungwe sheria ndogo, kushinikiza wanaume kushiriki huduma ya kliniki kwa lazima.
soma zaidi...........


Wametaka sheria itungwe ili atakayekaidi, achukuliwe hatua za kisheria na kupata adhabu kali. Walisema kuwepo kwa sheria hiyo, kutapunguza idadi ya wanawake wanaokwenda kliniki peke yao, na kusaidia wajawazito kupata huduma mbalimbali.

Walitoa mapendekezo hayo kwenye semina, iliyowahusisha madiwani na watendaji wa kata wa wilaya ya Itilima. Semina hiyo iliandaliwa na Shirika la Utafiti Afya (AMREF ) juu ya utoaji wa huduma ya afya ya uzazi na mtoto.

Katika semina hiyo, waliazimia kuwepo mfuko maalumu ndani ya halmashauri yao, ambao utatakiwa kuwekewa bajeti ya kutosha kuhudumu jamii husika kwa wakati na haraka 

“Wanawake wanatakiwa kuwahamasisha waume zao kushiriki kila mara huduma za kliniki pindi wanapokuwa wajawazito na kuondokana na mila potofu kushiriki huduma hiyo, "alisema.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Beatus Chikoti alisema jamii hasa wanaume, wamekuwa na fikra potofu kuwa mwanaume akishiriki kliniki ni jambo linaloleta aibu.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...