Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria |
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amesema kuwa, Waislamu nchini humo
hawabaguliwi na kwamba serikali inaamiliana nao kama ilivyo kwa raia wa
dini nyingine.
Taarifa ya ikulu ya Rais iliyotolewa kwa vyombo vya habari na msemaji wa
Rais imekanusha tuhuma za kuweko muamala wa kibaguzi unaofanywa na Rais
wa nchi hiyo dhidi ya Waislamu.
Reuben Abati, msemaji wa Rais Goodluck Jonathan amebainisha kwamba,
serikali ya Rais Jonathan haiamiliani na raia wa nchi hiyo kwa misingi
ya dini na kwamba, tuhuma za kufanywa ubaguzi dhidi ya Waislamu hazina
ukweli wowote.
Wakati serikali ikitoa taarifa ya kukanusha madai hayo, wapinzani
wameendelea kusitiza kwamba, Waislamu nchini Nigeria wanabaguliwa.
Nassir Rafai, kiongozi wa chama cha upinzani cha All Nigeria Peoples
Party amesisitiza kwamba, rais Jonathan amekuwa akiamiliana na wananchi
wa nchi hiyo kwa misingi ya kidini na ukabila. Waislamu nchini Nigeria
wanaunda asilimia 62 ya wakazi milioni 170 wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment