
Sehemu iliyozungushiwa duara jekundu kulia inamuonyesha Thiago akiwa amevaa jezi ya Man United enzi za utoto wake.
Barca ambao awali walikuwa wazito kuzungumza na United juu ya usajili wa Mchezaji huyo kwa kuwa wanamtazama kama mrithi sahihi wa nafasi ya kiungo Xavi Hernandez lakini kwa hatua iliyofikia hawana jinsi zaidi ya kukubali kwa kuwa tayari mchezaji mwenyewe amefanya maamuzi ya kuondoka.
Tayari makubaliano ya kimsingi baina ya Mchezaji (Thiago Alcantarra) na Manchester United yamefanyika ambapo inaaminika kuwa mchezaji huyo atasaini mkataba wa miaka mitano ndani ya United kwa thamani ya Euro milioni 18.
Barcelona wanaonekana kukata tamaa ya kubaki na mchezaji huyo kama zinavyoonyesha baadhi ya ishara ikiwemo taswira ya mchezaji huyo kuondolewa kwenye picha ya uzi duzi wa jezi mpya za klabu hiyo ya Hispania,namba ya jezi aliyokuwa anaivaa ( jezi namba 11) kupewa kwa mchezaji mwingine ambaye ni Neymar huku kukiwa na ripoti kuwa baba mzazi wa mchezaji huyo ambaye ni nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Mazinho kuuza mgahawa wa familia ulioko huko Catalunya zote hizi zikiwa ishara ya kujiandaa na maisha nje ya Hispania.
Endapo United itafanikiwa kumsajili mchezaji huyo atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa baada ya nyota wa timu ya taifa ya Uruguay Under-21 Guilermo Varela kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na David Moyes kama kocha mpya wa United.
No comments:
Post a Comment