facebook likes

Monday, July 8, 2013

Cheka kidogo hapa mtu wangu wa nguvu upate starter ya jumatatu na wiki nzima.

a.baa-Its-monday-again...

Mtu wangu wa nguvu wiki ndiyo imeshaanza na jumatatu ndiyo hii. Najua wengi monday ni siku ngumu sana hasa pale unapotafuta energy ya kurudisha hali ya kazi. Basi kama vipi nakupa vipande hivi vya vichekesho ambavyo vitakupa starter nzuri ya jumatatu yako mtu wangu wa nguvu na uendelee na kazi kama kawaida
Kimombo na sms, Jamaa katumiwa meseji na girlfriend wake. Kutokana na urefu wa meseji hiyo ikashindwa kufika yote,  mwishoni ikaandika some text missing. Jamaa kizungu hajui hivyo maneno ya mwisho hakuelewa maana yake lakini akahisi litakuwa neno la kimahaba, kujifanya aonekane mjanja akajibu.. “some text missing too dear”
………….
Kuna majambazi walifanikiwa kuingia Bank na kuiba Pesa nyiingi sana na kufanikiwa kutoroka. Wakafika sehemu wakaanza kuzihesabu hadi wakachoka kuhesabu. Mmoja akawambia, “Oyaa mi nimechoka kuhesabu tusubiri taarifa ya habari itangaze tumeiba Sh Ngapi.”
…………
Baba: Mwanangu ehe, shika hii shilingi 500 usimuambie mama yako kuwa nimelala na housegirl.
Mtoto: Sitaki, tatizo we baba ni mbahiri sana mwenzio mama akilala na dereva ananipaga shilingi 1,000
…………
WAZO LA JUMATATU
Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mshahara.
Masista doo watavaa vimini vyote lakini sio mini kabaang
…………
Mke: kuna nini kwa jirani??
Mme: kutakuwa kuna birthday..
Mke:ya nani??
Mme:itakuwa ya TUYU
Mke: TUYU ndo nan?
Mme: sijui ndo nani nimesikia wanaimba Happy birthday Tuyu,
………..
Mjukuu akamnon’goneza Babu, “Naomba mia tano”. Babu alikua hana kitu akajifanya hajasikia ninong’oneze sikio la huku hilo bovu. Mjukuu akamnong’oneza kwenye sikio lingine “Babu naomba elfu tano”. Babu akahamaki nooo huku ndio sisikii kabisaaa bora kule ulikoomba mia tano nadhani ntasikia! mjukuu hoi!.
………
Jamani uoga huu….!!!
Familia moja ilivamiwa na majambazi basi ilikua hivi.
JAMBAZI:wewe mama unaitwa nani.?
MAMA:mimi naitwa ASHA
JAMBAZI:una bahati sana jina lako kama la marehem mama yangu hivyo sikuui….,
na wewe baba unaitwa nani…?
BABA:mimi naitwa ATHUMANI lakini kazini wamezoea kuniita ASHA kama marehemu mama yako
……….
Mwalimu Alisimama Darasani Akauliza
Mtu Ambaye Mjinga Asimame…Madenge Akasimama Peke yake
Mwalimu: Wewe ndo Mjinga???..
Madenge: Nimeona nisimame Usiwepeke yako..
………
Mke alifariki dunia akakutana na mumewe mbinguni ,mke akamwambia mumewe” mume wangu bora tumekutana tuendeleze mapenzi yetu” mume akajibu tuliapa kifo ndo kitatutenganisha huku mbinguni nipo single na kuna malaika namfukuzia kwahyo usinijue!
………..
Jamaa kamdanganya girlfriend wake kuwa anasomea HOTEL MANAGEMENT.
Siku huyo girlfriend akamkuta jamaa anaosha vyombo kwa MAMA NTILIE.
Girlfriend akamuuliza jamaa “beby vipi mbona uko hapa?”
Jamaa bila woga akajibu “NIPO FIELD”.
………….
source: millardayo

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...