Mwanadada toka UFaransa Marion Baroli ameweka historia ya kuwa
mwanamke wa 18 kutwaa ubingwa wa michuano ya tenis ya Wimbledon
akimshinda Mjerumani Sabine Liscki .
Bartoli ambaye alishinda kwa seti mbili bila majibu akishinda kwa
michezo 6-1 na 6-4 aliweka historia nyingine ya kuwa mwanamke pekee
kutwaa ubingwa wa Wimbledon bila kucheza na mchezaji aliyeko kwenye top
10 ya viwango vya Ubora duniani Huku pia akiwa mchezaji wa kwanza ambaye
hayuko kwenye top 10 kutwaa ubingwa katika historia ya michuano hiyo.
Sabine Licki alionekana kuzidiwa tangu mapema kiasi cha kuanza
kububujikwa machozi kabla ya mchezo kuisha hali iliyomfanya apoteze
mwelekeo na kupoteza mchezo huo. Mwanadada huyo ameondoka na kitita cha
dola milioni 1.6 kama zawadi ya kutwaa ubingwa huo .
Fainali hiyo kwa upande wa wanaume itafanyika hapo kesho ambapo Andy Murray wa Scotland atacheza na Novak Djokovic wa Serbia .
No comments:
Post a Comment