facebook likes

Monday, February 18, 2013

WANIGERIA WANAZIDI KUFANYA KOLABO NA WAMAREKANI, HUYU NI MWINGINE

Huyu mwimbaji anaitwa Olu Maintain, ni Mnigeria ambae anaishi Marekani ambapo baada ya kina D’banj, P Square, J Martins na 2 Face kuhusika kwenye headlines kwa kolabo na wanamuziki wa Marekani, yeye ndio amechukua headlines sasa hivi baada ya video yake kutoka akiwa anarekodi studio na Olivia member wa zamani wa G Unit.
J Martins aliwahi kuingia kwenye headlines kwa kufanya kolabo na Pitbull lakini inaaminika kolabo hiyo imeshindwa kufanyika kutokana na staa huyo kumwambia J hataki kulipwa kwa kolabo ila anachotaka ni kuandaliwa show Africa ambayo gharama yake ni zaidi ya dola za kimarekani laki moja ambayo ni pesa ndefu sana.
2 Face alionekana na Mary J lakini mapaka leo sijui iliishia wapi ile stori, kwa sasa ni hayo tu… acha nikuache umtazame Olu Maintain hapa chini akiwa na Olivia.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...