facebook likes

Monday, February 18, 2013

BREAKING NEWS:JENGO LA GHOROFA TANO LAPOROMOKA NA KUSABABISHA KIFO CHA MTU MMOJA MAENEO YA SINZA


 Picha hii si ya tukio lenyewe

Jengo kuu la Ghorofa 5 ambalo lilikuwa halijamalizika ujenzi wake lililopo eneo la Sinza Mori karibu kabisa na Masjid Qubah,limeporomoka jana na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye alikuwa na wenzake wawili jirani na jengo hilo,ambapo mmoja alivyoona hatari hiyo alikimbia na kuwaacha wenzie wawili ambao walinasa ndani.

Kati ya walionasa mmoja amefanikiwa kutolewa huku akiwa ameumia vibaya na mwingine ndio huyo aliepoteza maisha.

Inasemekana chanzo cha kuanguka kwa jengo hilo la Ghorofa ni hali yake ya kukaa kwa muda mrefu bila kumalizika kwa ujenzi waka ambapo inadaiwa kuwa lina umri wa zaidi ya miaka 10. 

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...