facebook likes

Monday, February 18, 2013

Diamond ataja sababu ya kuvuja kwa wimbo wake mpya wa ‘Ukimwona’

Inasemekana Msanii wa Bongofleva, Diamond Platnumz ametoa sababu ya kuvuja kwa wimbo wake huo wa 'Ukimwona' kwenye mitandao mbalimbali hapa Bongo

Inasemekana Ngoma hiyo inasikika pia kwenye Clubs huku Diamond mwenyewe akikiri kwamba anaombwa na mashabiki zake auimbe akiwa kwenye Shows zake. Diamond ametoa sababu ya kuvuja kwa Ngoma hiyo na kusema;

Wimbo huo haukua umekamilika, meaning it's a Demo ambayo ilikua kwenye Playlist ya Simu yake aina ya Blackberry, simu ambayo aliiweka kwenye moja ya magari yake. 

Inasemekana aliipoteza simu hiyo wakati anatoka nyumbani kwake akielekea Magomeni, ambapo ali-notice kwamba simu yake haipo wakati yupo kariakoo. Ila anaamini ni mipango ya Mungu na anafurahia jinsi wimbo huo unavyofanya vizuri.

'Ukimwona' ni ngoma mpya ya Diamond ambayo imeanza kusikika wiki iliyopita baada ya kuwa uploaded kwenye mitandao mbalimbali ya hapa Bongo. Isikilize hapa kama bado hujaisikia.



No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...