Mmoja wa mapadre waandamizi wa kanisa
katoliki nchini Uingereza amejiuzulu wadhifa wake kufuatia shutma za
kwamba alikwenda kinyume na matakwa ya kipadre mapema miaka ya
themanini.
Kardinal Keith O'Brien ameachia madaraka kama
kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchini Scotland na hatarajii kusafiri
kwenda Vatican baadaye mwaka huu kumchagua Papa ajaye baada ya baba
Mtakatifu Benedict wa 16 kijuzulu.
BBC imeelezwa kuwa kiongozi
huyo,ameshutumiwa na mapadre watatu wa kanisa hilo na hatua hiyo ya
kujiuzulu ni tukio kubwa katika mwenendo wa kanisa katoliki ikizingatiwa
kuwa Kanisa hilo limekuwa kwenye shutuma za ulaji rushwa na matatizo ya
kiongozi kwa siku za hivi karibuni.
Inaarifiwa Padre O'Brien aliwauvinjia heshima makasisi mingo mitatu iliyopita.
Hata hivyo, mwishoni mwa wiki, alisema kuwa anapinga vikali madai hayo.
Duru zinasema kuwa hatua ya kujizulu kwa padre
huyo kunaongeza shinikizo kwa makadinali wengine wanaokabiliwa na tuhuma
za walivyoshughulikia kashfa za ngono
na BBC
No comments:
Post a Comment