facebook likes

Tuesday, February 26, 2013

FILAMU YA ' LIFE OF PI' YAVUNJA REKODI TUZO ZA OSCARS



Filamu ya 'Life of Pi' imevunja rekodi kwa kushinda  tuzo nne za 'Oscars Academic' zilizofanyika jana usiku huku filamu ya 'Argo' ikiwa imenyakua tuzo tatu ikifwatiwa na 'Django Unchained' kwa kunyakua tuzo mbili

Life of Pi imeonekana kuvunja rekodi zaidi kwa kuwa ni filamu  ya pekee kutajwa mara 11 katika vipengele vyote 24 na kuweza kunyakua tuzo nne ikiwemo tuzo ya muongozaji bora,muziki wa asili,'Visual effects' na 'cinematography'

Ang Lee ambaye ndiye aliyechukua tuzo ya muandaaji bora kwa kupitia filamu yake ya Life of Pi imeonyesha utofauti mkubwa kwa kuweza kumuangusha Steven Spielberg ambapo kila mwaka alikuwa anaongoza kwa kuchukua tuzo hiyo hali ambayo kwa sasa imeonekana kuwa tofauti

Nayo filamu ya Argo imetajwa kwenye vipengele 7 na kuweza kunyakua tuzo tatu ikiwemo tuzo ya filamu bora, uhalili wa filamu pamoja na uandishi bora

Huku tuzo ya 'Actor in a suppoting role' ikiwa imechukuliwa na Christoph Waltz katika filamu ya 'Django Unchained' pamoja na tuzo ya uandishi bora ikichukuliwa na Quentin Tarantino katika filamu hiyo hiyo ya 'Django Unchained'

Ingawa filamu ya Lincoln imeonekana kutajwa mara 12 katika vipengere 24 imeweza kunyakuwa tuzo moja katika kipengele cha Usanifu Utayarishaji

Tuzo za Oscars Academic ni tuzo zinazofanyika kila mwaka ambapo sasa ni mara ya 85 kufanyika tuzo hizo

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...