JESHI
la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia watu 13, wakiwemo askari wawili wa
Jeshi la wananchi (JWTZ) na polisi mmoja
kwa matukio ya mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha.
Akizungumza
na waandishi habari jijini Mbeya Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athuman amesema watuhumiwa hao
wamewagawanya katika makundi mawili, ambapo kundi la kwanza ni la watuhumiwa 9
wakiwemo askari hao wawili wakidaiwa kuhusika na tukio la kuwaua kikatili na
kisha kuwazika dereva na utingo wake.
kundi
la pili ni la watuhumiwa wanne wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya dereva wa
polisi lililotokea Wilayani Chunya mkoani hapa baada ya kufanyika uporaji wa
shilingi milioni 2,200,000 katika kituo cha mafuta eneo la Matundasi wilayani
chunya.
Akitoa
ufafanuzi zaidi Kamanda Diwani amesema, katika tukio la kwanza ni lile
lililotokea Februari 2 katika eneo la Mafinga,Mkoani Mbeya, ambapo watuhumiwa
wa kundi la kwanza waliwateka dereva na utingo wake, Festo Kyando (45) na
Jafari lililotokea na kuwaua kisha kwenda kuwazika porini.
Amesema
dereva huyo alikuwa ametoka Jijini Dar es salaam kubeba mzigo wa
wafanyabiashara kwa lengo la kuleta mkoani Mbeya, lakini kumbe walikuwa
wakiwindwa na walipofika mkoani Iringa walitekwa na kufanyiwa mauaji hayo ya
kinyama.
Kamanda
Diwani amesema kufuatia tukio hilo jeshi la polisi lilianza uchunguzi mkali na
hatimaye kunasa mtandao huo wa watu 9 wakiwemo askari hao wawili wa jeshi la
polisi na JWTZ,ambao uchunguzi umebaini kuwa hutoa mavazi ya majeshi hayo na
silaha.
Kamanda
Diwani amewataja watuhumiwa hao kuwa MT.85393 Samwel Charles Balumwina(31) wajiriwa wa jeshi la
wananchi kikosi 844 kikosi cha Itende Mbeya na G.1901PC Samwel Kigunye (27)
askari wa jeshi la polisi Jijini Mbeya.
Wengine
ni mfanyabiashara maarufu wa eneo la Mwanjelwa, Gath Mbilinyi (32), Rajabu
Mbilinyi(25), Gregory Mtega(25,Francis Sanga(30) pamoja na ndugu ambao ni
wafanyabiashara maarufu katika mji wa Makambako mkoani Njombe ambao ni Japhet
Ng'ang'ana(24), Claud Ng'ang'ana(36), Hilally Ng'ang'ana(30)
Hata
hivyo amesema walifanikiwa kukamata bidhaa hizo katika eneo la Tunduma ambako
tayari zilikuwa zimekamatwa na kwamba miongoni mwa watuhumiwa ndiye aliyeuziwa
mzigo huo.
Amesema
mali zilizookolewa katika matukio hayo kuwa ni Nondo 397 za aina tofauti pamoja
na bando 18 za mifuko ya sandarusi(Sulphate) ambavyo vinashikiliwa na jeshi la
Polisi Tunduma Wilani Mbozi Mkoani hapa.
Katika
tukio la pili ni lile linalohusisha vifo vya watu wawili wilayani Chunya, ambao
ni dereva wa polisi na dereva wa gari la majambazi baada ya kutokea kurushiana
risasi.
Amesema
tukio hilo lilitokea Februari 6 baada ya watuhumiwa wanne ambao wanashikiliwa
na jeshi hilo kufanya uporaji wa shilingi milioni 2,200,000 katika kituo cha
matundasi wilayani humo.
Amewataja
madereva hao waliouwawa katika tukio hilo kuwa ni dereva wa polisi
aliyefahamika kwa jina moja la Jafari, ambapo yule wa majambazi akitajwa kwa
jina la Shabani John.
Diwani
amewataja watuhumiwa wanashikiliwa kwa tukio hilo kuwa ni Manase Kibona
(37).Emmanuel Mndendemi na Masai Hongole, Mashaka George, John Mahenge, Narasco
Mabiki.
Kamanda
huyo amezitaja mali zilizookolewa katika matukio hayo kuwa ni Nondo 397 za aina
tofauti pamoja na bando 18 za mifuko ya sandarusi(Sulphate) ambavyo
vinashikiliwa na jeshi la Polisi Tunduma Wilani Momba Mkoani Mbeya.
Aidha,kamanda
Diwani amevitaja baadhi ya
vielelezo vilivyokamatwa kuwa ni
Bunduki aina ya Shot Gun moja ambayo namba zake zilifutika, Gobore moja ambalo
pia namba zake zilifutika, Bastora tatu zilizotengenezwa kienyeji zisizo na
namba na zinazotumia risasi za s/Gun.
Vingine
ni Risasi 31 za Silaha ya SMG/SAR, Sare za Jeshi (JWTZ), suruali 4, mashati 4
kofia 3 na Viatu jozi mbili , Risasi 99 za S/GUN, Risasi 25 za Bastola na
magari yenye namba T 464BLX TOYOTA COROLA,T381 BDR VITZ, T 251 AKU Toyota Pick
Up ,T 193 BDY Toyota Premio na T
214 ASV Toyot Mark II.
Hata
hivyo Kamanda wa Polisi anawashukuru wananchi wa Mkoa wa Mbeya waliojitokeza
katika ktoa ushirikiano wa kuwasaka majambazi hayo ambapo pia anaendelea kutoa
wito kwa watu wenye taarifa za watu ambao haeajakamatwa.
Ameongeza
kuwa taratibu za upelelezi zimekamilika ambapo taratibu za kuwafikisha
mahamakamani zinaendelea.
|
No comments:
Post a Comment