facebook likes

Thursday, February 7, 2013

MKUU WA IDARA YA VIPINDI CLOUDS AFUNGUKA KWA WATENGENEZA MATANGAZO YA BIASHARA YA REDIO


 Masaa kadhaa yaliyopita, kupitia ukurusa wake wa facebook, mkuu wa idara ya vipindi kutoka Clouds Fm, bwana Sebastian maganga, aliandika ujumbe mahsusi kwa wahusika wa matangazo ya biashara hasa hasa matangazo ya redio, ikiwa ni muendelezo wa tabia yake ya kujuza na kuelimisha kupitia ukurasa wake huo wa facebook, pale anapoona kuwa na uelewa wa jambo flani, na kwa namna moja ama nyingine akijaribu kutoa elimu aliyonayo juu ya jambo hilo
UJUMBE KWA WATENGENEZAJI WA MATANGAZO YA BIASHARA YA REDIO:"SIO SWALA LA UJIKO, NI SWALA LA KUTOA SULUHISHO"

MFANO WA UJIKO: sisi ni kampuni bora ya kutengeneza gesi kwa kutumia maganda ya ndizi kwa zaidi ya miaka 15.

MFANO WA KUTOA SULUHISHO: gesi bora kwa ajili ya matumizi yako ya kila siku nyumbani, kwa gharama nafuu, hiyo ndio ahadi yetu kwako.

UJIKO AU UZOWEFU WA KAMPUNI HAUMHUSU MTEJA, SULUHISHO LA BIDHAA AU HUDUMA YA KAMPUNI HUSIKA NA NAMNA INAVYOATHIRI MAISHA YA MTEJA NDIO JAMBO MUHIMU, SIJUI MMENIPATA HAPO

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...