KWA WAPENZI WA MOVIE, HII NDO MOVIE MPYA KUTOKA KWA MAMA KANUMBA, INAITWA "WITHOUT DADDY."
MAMA
Mzazi wa msanii nyota Tanzania marehemu Steven Kanumba ‘Kanumba’ Frola
Mtegoa ameigiza filamu katika muendelezo wa kipaji cha mwanaye baada
ya kuigiza katika filamu ya Without Daddy akishirikiana
na watoto waliokuwa wakiigiza na marehemu Kanumba kama Patrick na
Jamila, katika filamu hiyo mama Kanumba kaigiza katika kiwango cha juu.
.
Ben Blanco akiwa na wasanii wakali Jamila na mwenzake.
Akiongea na FC mkurugenzi wa kampuni ya Big Daddy Production Irene Kaungwa amesema kuwa filamu ya Without Daddy ni kazi mwendelezo wa kazi ya marehemu Kanumba iliyotoka siku za nyuma ya Big Daddy
na ni kazi ambayo imetentengezwa kwa ubora wa kimataifa ikiwa sambamba
na kumtambulisha mama Kanumba katika tasnia ya filamu Swahiliwood.
“Kampuni
ya Big Daddy Production imekusudia kuleta mapinduzi makubwa katika
tasnia ya filamu Tanzania, na katika kumuenzi marehemu tumemchukua mama
Kanumba kushiriki katika filamu hiyo na mama ameonyesha uwezo mkubwa
katika uigizaji na filamu yake ya kwanza
ndio hii,”anasema mkurugenzi.
.
Mmoja kati ya wasanii walioshiriki katika Filamu ya Without Daddy.
Mama Kanumba mwigizaji.
Filamu
ya Without Daddy imeshirikisha wasanii nyota wengi kama vile Abdalah
Mkumbilah ‘Muhogo mchungu’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’ Cathy Rupia,
Mayasa Mrisho, ‘Maya’, Othuman Njaidi ‘Patrick’ Wastara Juma ‘Stara’
Abdul Ahmed ‘Ben Blanco’ na wasanii mahiri wengineo.
No comments:
Post a Comment