UINGEREZA
jana usiku ilifanikiwa kupata ushindi wa kwanza dhidi ya Brazil tangu
mwaka 1990 kufuatia ushindi wa mabao 2-1 ndani ya dimba la Wembley
yaliyofungwa na Wayne Rooney na Frank Lampard.
Ikiwa
ni mechi maalum ya kusherehekea miaka 150 ya chama cha soka Uingereza
(FA), iliwachukua wenyeji dakika 26 kupata bao la kuongoza kupitia kwa
Wayne Rooney baada ya kipa Julio Cesar kuutema mkwaju wa chini wa Theo
Walcott.
Rooney akipiga bao la kwanza
Brazil
wangeweza kuongoza mapema baada ya refa Pedro Proenca wa Ureno
kuwazawadia penalti dakika ya 19 kufuatia kiungo Jack Wilshere kuunawa
mpiria wa krosi ya Ronaldinho.
Lakini Ronaldinho, Supa staa wa zamani wa Barcelona, alishuhudia mkwaju wake wa penalti ukiokolewa na kipa Joe Hart.
Ronaldinho akikosa penalti
Kocha
Hudgson wa Uingereza alifanya mabadiliko mawili wakati wa mapumziko kwa
kuwatoa Tom Cleverley aliyempisha Lampard na Ashley Cole aliyepokelewa
na Leighton Baines.
Lakini
ni mabadiliko ya Brazil ndio yaliyoanza kuzaa matunda baada ya mcheaji
aliyetokea benchi, Fred kuwasawazishia wageni dakika ya 49 kufuatia
uzembe wa beki Gary Cahill aliyeshindwa kuumiliki vizuri mpira mbele ya
Luis Fabiano.
Frank Lampard akaibuka shujaa kwa bao lake la dakika ya 60 kufuatia pasi ya Wayne Rooney.
Hii
inakuwa ni mara ya kwanza kwa England kupata mabao mawili dhidi ya
Brazil tangu mwaka 1984 iliyoshuhudia bao la kukumbukwa la John Barnes.
Katika
mechi ya jana, Ronaldinho alizawadiwa jezi maalum ya kutimiza kwake
mechi 100 katika timu ya taifa huku Steven Gerrard naye akikabidhiwa tuzo ya dhahabu na kipa wa zamani Peter Shilton kwa kutimiza mechi 101.
Ronaldinho akipokea zawadi ya kutimiza mechi 100
Gerrard akipokea zawadi ya kutimiza mechi 100
Katika
mechi nyingine kubwa za kirafiki zilizochezwa jana, Ujerumani iliichapa
Ufaransa 2-1, Argentina ikashinda 3-2 dhidi ya Sweden, Uholanzi
wakatoka 1-1 na Italia huku Hispania ikiichabanga Uruguay 3-1.
No comments:
Post a Comment