MAKAMU Mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward ameondoka ghafla jana kwenye kambi ya maandalizi ya msimu ya klabu nchini Australia kwenda kushughulikia usajili wa kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas.
United bado inajiamini itapata huduma za Fabregas, licha ya mchezaji huyo wa Barca kusema kwamba anataka kubaki Nou Camp na Arsenal inapewa kipaumbe cha kumsajili kwa Pauni Milioni 25 Nahodha wao huyo wa zamani.
Vyanzo kutoka kambi ya mabingwa hao wa Ligi Kuu England vinasema Fabregas atajiunga nao, ingawa itawagharimu zaidi ya Pauni Milioni 26 walizotoa kama ofa ya kumtaka mapema wiki hii.
Anatakiwa: Manchester United inamtaka Nahodha wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas
Fabregas aliichezea Arsenal kuanzia mwaka 2003 hadi 2011, lakini amekuwa akiipenda klabu hiyo ya Old Trafford kwa muda mrefu.
Akizungumza na gazeti la Sunday kuelekea Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Arsenal na United mwaka 2009, Fabregas alisema: "Mimi shabiki mzuri wa Man United. Sina tatizo kusema United ni moja ya klabu bora duniani – ingawa pia ninataka kuwafunga. Wao ni timu bora duniani kwa sasa – wa juu, timu ya juu na tunawaheshimu kwa kiasi kikubwa.'
Kuondoka kwa Woodward kunakuja siku moja na kauli ya United kukataa ofa ya Chelsea kwa ajili ya mshambuliaji Wayne Rooney - mchezaji ambaye kocha David Moyes amesistiza hauzwi.
Hadi sasa mchezaji pekee ambaye amesajiliwa ni beki kinda wa timu ya taifa ya Uruguay chini ya miaka 20,Guillermo Varela, ambaye hata hivyo hajaripoti kazini bado.
Thiago Alcantara na Kevin Strootman, ambao wote walikuwa wanatakiwa sana United, wameamua kujiunga na Bayern Munich na Roma na kumuacha Moyes akiwa katika mahitaji ya kusaini viungo kikosini mwake.
No comments:
Post a Comment