Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na
“Wizara inaomba sote tuitafakari na kuitekeleza dhana ya
Jeshi la Polisi
ya Ulinzi Shirikishi ni muhimu kila mwananchi mzalendo wa
nchi hii ashiriki kikamilifu kudumisha amani na ulinzi wa nchi na rasilimali
zake zote”Alisema Yustina.
Aidha Yustina alisema ulindaji wa rasilimali hizo hasa
wanyama pori utasaidia kujenga na kuimarisha utalii wa nchi kutokana na zaidi
ya asilimia 90 utalii unategemea wanyamapori na hivyo kuingizia nchi fedha za
kigeni na pia kukuza uchumi.”Kwa hapa nchini zaidi ya asilimia 90 ya utalii
unategemea wanyama pori hivyo, watalii wengi huja kuwaona, kuwapiga picha na
kuondoka wachache huja kuwawinda kisheria na kuchukua nyara. Wanyamapori ndio
wamebeba utalii katika Tanzania na kwa maana hiyo ndio, kwa kiasi kikubwa,
wamebeba uchumi wa nchi hii” Alisema Yustina.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Kuzuia Ujangili kutoka
wizara hiyo Bw. John Muya aliwataka
wananchi waliokatazwa kuishi maeneo ya njia za wanyama kutekeleza agizo hilo
ili kuepuka uharibifu unaofanywa na wanyama hao kipindi cha uhamiaji.“Napenda
kutoa wito kwa wananchi kuondoka kwenye yale maeneo ambayo ni mapito ya wanyama
pindi wanapohama kuondoka ili kuondoa usumbufu na uharibifu wa mali” Alisema
Muya.
Yustina aliwataka wananchi kuacha kuwatazama baadhi ya
wanyama kama Fisi na Tembo kama kero kwa wananchi, badala yake tuwatazame
wanyamapori kama benki kubwa na kama mkombozi wa nchi yetu kiuchumi.
No comments:
Post a Comment