facebook likes

Thursday, July 18, 2013

CHELSEA SASA WATANGAZA OFA YA PAUNI MILIONI 30 KWA ROONEY


KOCHA Jose Mourinho amekiri wametoa ofa kwa ajili ya Wayne Rooney na habari zinasema wamesema wataipa Manchester United hata Pauni Milioni 30 wamnase nyota huyo.
Ndani ya saa 24 tangu vyanzo vya karibu na Rooney kufichua kwamba ‘ana hasira na amechanganyikiwa’, mshambuliaji huyo yuko tayari kuwasilisha barua ya kuomba kuondoka, kwa sababu kocha David Moyes amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hatakuwa mshambuliaji chaguo la kwanza.
Chelsea ilianza kupeleka ofa ya Pauni Milioni 22 ambayo ilikataliwa na United na sasa wanarudi na ofa iliyonenepa, Pauni Milioni 25— jumla Milioni 3 na inaweza kupanda hadi Milioni 30, ili tu wampate mkali huyo. 
Ofa ya awali iliyofichuliwa na MailOnline na kukanushwa na Chelsea ilikuwa inahusi fedha na mchezaji kati ya Juan Mata na David Luiz.
We want Roo: Mourinho chats with Chief Executive Ron Gourlay
Tunamtaka Roo: Mourinho akizungumza na Mtendaji Mkuu, Ron Gourlay

United imekataa ofa ya awali ya Chelsea na kuwaambia wasithubutu kurejea tena, kwa sababu Rooney hauzwi.
Chelsea baadaye ikawatuhumu mabingwa hao wa Ligi Kuu England kwa kuvujisha taarifa za ofa ya awali.
Taarifa kutoka Stamford Bridge ilisomeka: "Chelsea FC inathibitisha kwamba jana (juzi) imeandika barua rasmi ya ofa kwa Manchester United kwa ajili ya kumsajili Wayne Rooney.
"Pamoja na hayo, vipengele vya ofa ni siri, kuepuka shaka na usumbufu uliotokana Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Sydney, mapendekezo ya dau hayahusishi uhamisho wa mkopo au mchezaji yeyote kutoka Chelsea kwenda Manchester United,". 
Transfer tussle: Wayne Rooney's future remains unclear
Sakata la uhamisho: Mustakabali wa Wayne Rooney bado tata

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...