facebook likes

Wednesday, October 9, 2013

Ronaldo sasa azama katika penzi la DJ

 RIO DE JANEIRO, BRAZIL
HAJAWAHI kukosea ndani na nje ya uwanja. Baada ya penzi lake la mkewe, Bia Anthony, kufa Desemba mwaka jana, mkongwe wa soka nchini Brazil, Ronaldo de Lima, ameibuka kivingine kabisa.
SOMA ZAIDI.........
Ronaldo ameanzisha uhusiano wa kimapenzi na DJ mrembo, Paula Morais, ambapo penzi lao linaonekana kushika chati nchini Brazil kama ilivyo ada kwa Ronaldo ambaye ni maarufu nchini humo.
Staa huyo wa zamani wa Barcelona, Inter Milan, Real Madrid na AC Milan, ameachana na mkewe aliyedumu naye kwa miaka saba na sasa inaonekana amezama katika penzi la Paula kiasi cha kufuatana naye kila mahali.
Penzi lao lilianza kudhihirika katika tamasha la Samba nchini Brazil hivi karibuni ambapo wawili hao walijitokeza hadharani na kuvutia umati wa mashabiki.
Kama vile haitoshi, Paula alitoa kiashirio kwamba yuko katika penzi zito na Ronaldo na kwamba anaiangalia afya ya nyota huyo kwa karibu hasa baada ya staa huyo kupunguza kilo 17 akifuata  mpangilio wa vyakula kwa mujibu wa kituo kimoja cha televisheni nchini Brazil.
Paula alituma picha ya Ronaldo akiwa ameshikilia kikaangio kilichokuwa na mayai ya kukaanga huku akiandika ‘Jiko ni sehemu ya Mwanamume, nakupenda.’
Kama vile haitoshi, siku za karibuni Ronaldo alisafiri na Paula mpaka nchini Hispania kwa ajili ya kula raha katika miji mbalimbali nchini humo. Walionekana wakiwa katika fukwe za maraha za Ibiza wakiponda starehe.
Pia walionekana wameshikana mikono katika Jiji la Madrid wakiwa katika maduka ya Chanel & Hermes wakifanya manunuzi huku wakipiga stori za mahaba.
Kama inavyoonekana pichani, Ronaldo pia amekuwa akiwa sambamba na Paula hadi katika sehemu yake ya kazi huku akivamia katika chumba cha MaDJ ambacho ni maalumu kwa wapiga muziki peke yao.
Huu ni mwendelezo wa Ronaldo katika harakati zake za kupenda vimwana ambapo penzi lake la awali na mkewe Bia, liliingia katika dosari baada ya Ronaldo kukumbwa na kashfa ya kuingia chumbani na wanaume wanne waliojibadili jinsia. Hata hivyo ndoa yao baadaye iliendelea baada ya Ronaldo kuomba msamaha.
Mtoto wao wa kwanza, Maria Sophia, alizaliwa Desemba 24, 2008. Mtoto wa pili, Maria Beatriz alizaliwa Aprili, 6 2010 na Mtoto wao wa tatu aliyepewa jina la Maria Alice, alizaliwa miaka 10 kamili tangu Ronaldo apate mtoto wake wa kwanza wa kiume.
Ronaldo ambaye pia alizaa na mkewe wa kwanza, Milene Domingues, Aprili 6, 2000. Ndoa yao ilidumu kwa kipindi cha miaka minne tu baada ya Milene kugundua tabia za kifuska za Ronaldo.
Kabla ya hapo, Ronaldo alikuwa katika uhusiano mzito wa kimapenzi na mwanamitindo mrembo mwigizaji, Susana Werner,  ambaye alikutana naye mwaka 1997 kabla ya kuwa naye katika uhusiano wa muda mrefu kiasi cha kwenda kuishi naye jijini Milan wakati akiichezea Inter Milan.
Ronaldo pia aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo maarufu wa Brazil, Daniela Cicarelli, ambaye alimpatia mimba lakini ikatoka.
Uhusiano wake na mrembo huyu ulidumu kwa miezi mitatu tu licha ya Ronaldo kumvalisha pete ya uchumba katika ukumbi wa kifahari Chateau de Chantilly ambapo gharama za tukio hilo liligharimu kiasi cha Pauni 700,000.
Desemba mwaka huo, Ronaldo alifanya vipimo vya DNA na kuthibitisha kwamba alikuwa baba wa mtoto, Alexander, aliyezaliwa Aprili 2005.
Mtoto huyo alitokana na uhusiano wa muda mfupi kati ya Ronaldo na Michele Umezu ambaye ni mhudumu wa baa na walikutana kwa mara ya kwanza jijini Tokyo katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002.
Baadaye Ronaldo alikiri kwamba alikuwa anataka kufunga uzazi kwa madai kwamba watoto wanne walikuwa wanamtosha, lakini hapo hapo akajikuta akipata mtoto wa tano na Bia ambaye alikuwa wa tatu kwao.
Kwa sasa Ronaldo anatarajiwa kuwa bize na shughuli za maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika nchini kwao Brazil Juni mwakani huku akiwa amechaguliwa kuwa miongoni mwa mabosi wa shughuli yenyewe.
Ronaldo pia anatazamiwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Brazil baada ya kuondoka madarakani kwa Rais wa sasa, Ricardo Teixeira, mwakani.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...