facebook likes

Sunday, September 22, 2013

CHELSEA YAIFUNGA FULHAM 2-0, KWENYE ENGLISH PREMIER LEAGUE , OSCAR NA MIKEL WAIPANDISHA KILELENI KWA MUDA


 

John Mikel akiambatana na wenzake kushangilia ushindi walioupata!

SOMA NA ANGALIA PICHA ZAIDI....

Jose Mourinho akiiongoza timu yake ya Chelsea kwenye uwanja wao Stanford Bridge kipindi cha kwanza kimemalizika timu zote zikiwa bado hazijafungana. Huku Chelsea wakiongoza mashambulizi zaidi ya Fullham, Mchezaji matata anayekubalika na Jose Oscar kipindi cha pili Chelsea wakifanya mashambulizi ya hatari wakaweza kupata bao dakika ya 52 kupitia Oscar baada ya kipa wa Fullham kufanya makosa ya kutema mpira. Dakika ya 84 Mikel akaipatia bao la pili Chelsea baada ya kupokea krosi safi kama kona na hatimaye kuunganisha moja kwa moja hadi nyavuni.

Jose Mourinho akitazama mtanange kipindi cha kwanza huku akiwa mambo yake na alivyopanga yakiwa bado magumu.
Mtanange ukiendelea!!Majanga!! Gary Cahill na Scott Parker chini hapa!Andre Schurrle akichuana na Steve Sidwell kipindi cha kwanza.
Oscar akishangilia baada ya kufunga bao kipindi cha pili.

Oscarakishangilia baada kuifungulia mlango Chelsea!

Oscar alivyoachia shuti golini na kuiwezesha timu ya Chelsea kushinda kuwaamsha mashabiki Stamford Bridge baada ya muda mrefu tangu kipindi cha kwanza baada ya Fullham kubana.

John Obi Mikel akimaliza ukame wake hapa baada ya kucheza mechi nyingi bila bao na hapa akitupia bao la ukweli!!

Jose Mourinho hakuwa na hamu pamoja na kushinda kwake hapa baada ya vipigo

Bosi wa Chelsea mwenye timu Roman Abramovich akijionea timu yake ikipata ushindi baada ya mwezi kupita bila ushindi.
Samuel Eto'o leo ameshindwa tena kuonesha cheche zake

John Terry kwenye patashika kusaidia timu ishinde

Branislav Ivanovic akiangushwa chini na Pajtim Kasami

Ramires, akijaribu kumkaba kwa nyuma Alexander Kacaniklic

Hazard akijaribu kufunga hapa na shuti lake kuelekea nje


RATIBA/MATOKEO
Jumamosi 21 Septemba
14:45 Norwich City  0 v  1 Aston Villa
17:00 Liverpool 0 v 1 Southampton
17:00 Newcastle United 2 v 3 Hull City
17:00 West Bromwich Albion 3 v 0 Sunderland
17:00 West Ham United 2 v 3 Everton
19:30 Chelsea 2 v 0 Fulham


Jumapili 22 Septemba
15:30 Arsenal v Stoke City
15:30 Crystal Palace v Swansea City
18:00 Cardiff City v Tottenham Hotspur
18:00 Manchester City v Manchester United

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...