facebook likes

Sunday, September 22, 2013

JK ATUNUKIWA SHAHADA YA UZAMIVU YA CHUO KIKUU CHA GUELPH JIMBONI ONTARIO, CANADA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Siku ya Ijumaa, Septemba 20, 2013, alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PHD) na Chuo Kikuu cha Guelph cha Canada kwa kutambua mchango na uongozi wake katika kuleta mageuzi ya kilimo katika Afrika.

SOMA ZAIDI....Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Chuo Kikuu Guelph baada ya kutunukiwa Shahada.
Viongozi wa Chuo hicho wamesema kuwa wamefanya uamuzi wa kumtunuku Rais Kikwete kutokana na jitihada zake za kukabiliana na changamoto zinazokabili kilimo, jitihada zake za kuleta usalama wa chakula na pia majaribio makubwa ya kuongeza matumizi ya technolojia katika kilimo cha Tanzania na Afrika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa Shahada ya Uzamivu na Provost na Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario, Dkt Maureen Mancuso.
Chuo cha Guelph ni moja ya vyuo vikuu vinavyoheshimiwa zaidi katika Canada na duniani katika Nyanja za kilimo na kilianzishwa rasmi kama Chuo cha Kilimo cha Jimbo la Ontario Mei Mosi, mwaka 1874. Soma zaidi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Guelph pamoja na na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario jana.

Umati ulioshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Wakuu wa Chuo Kikuu Guelph pamoja na na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario.

Picha kwa hisani ya sufianimafoto.com

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...