Mourinho anapeleka timu yake kuvaana na Manchester United leo na anataka kumvurua Moyes kuelekea mchezo huo wa kwanza wa ushindani kwake tangu arithi mikoba ya Sir Alex Ferguson.
Chelsea jana imethibitisha kumsaini Willian, na Samuel Eto’o yupo kwenye orodha pia kutoka Anzhi Makhachkala, lakini wameendelea komalia pia na saini ya Rooney na wanajiandaa kurejea na ofa iliyoboreshwa ya Pauni Milioni 30.
Mchezo wa lawama: Jose Mourinho amemsukumia lawama David Moyes kumvuruga Wayne Rooney (kulia)
Mtu wa kati: Mourinho angependa kumnunua Rooney kutoka Manchester United
Chaguo la pili: Moyes amemuambia Wayne Rooney ni chaguo la pili baada ya Robin van Persie
Moyes ameendelea kusistiza Rooney hauzwi na anaweza kucheza usiku wa leo, ingawa Mourinho anaamini bado anaweza kumnasa Rooney.
"Kwa nini?" alisema Mourinho, wakati alipoulizwa kama anatarajia mapoekzi mazuri kutoka kwa mashabiki wa United. "Wako dhidi yangu? Lakini sikusema utakuwa chaguo la pili kwangu.
"Tunajaribu kupata mchezaji mzuri ambaye Kocha atakuwa chaguo la pili kwake. Hatumfuati Van Persie. Hawatakiwi kuwa dhidi yangu. Ikiwa nilisema Ramires ni chaguo la pili kwangu na anacheza wakati Lampard amechoka, au majeruhi na ikiwa atatokea mtu kumchukua Ramires, hakuna atakayeshangaa,". Alipoulizwa kama lilikuwa kosa la Moyes, Mourinho alisema: "Ndio.’
Ilikuwa katikati ya Julai wakati Moyes aliposema: "Kwa ujumla fikra zangu juu ya Wayne ni, ni kwa sababu yeyote Robin van Persie ni majeruhi, tutamuhitaji,"alisema.
Hii ni kauli ambayo iliikera kambi ya Rooney, ambayo ilisema mchezaji huyo amekasirika na amechananyikiwa.
Anakuja: Mazungumzo yameanza juu ya Samuel Eto'o ambaye ni mpango B wa Mourinh
o
o
No comments:
Post a Comment