
Nyota kinda: Mchezaji mwenye thamani ya Pauni Milioni 50, Neymar aliingia kipindi cha pili na kufanya vizuri
KLABU ya Barcelona imepata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Malaga jana na kuendeleza mwanzo wao mzuri katika mbio za kutetea taji lao la La Liga.
Mabingwa hao walimkosa majeruhi Lionel Messi na ilisota kupata bao hilo pekee hadi beki wa pembeni Adriano alipokatiza upandd wa kulia kuingia ndani kabla ya kufumua shuti kali lililotinga nyavuni kabla ya mapumziko.
Mshambuliaji Mbrazil, Neymar aliingia kipindi cha pili na kuonyesha alistahili kuigharimu Barca Pauni Milioni 50.

Tofauti: Adriano akishangilia na wachezaji wenzake wa Barcelona baada ya kufunga

Hasira: Sergio Sanchez wa Malaga akionyesha hasira zake baada ya timu yake kukosa bao la wazi

Kasi: Alexis Sanchez wa Barca akimtoka Vitorino Antunes wa Malaga

Kazi kazi: Beki wa Malaga, Jesus Gamez alipewa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Neymar

Tabasamu: Gerardo Martino baada ya ushindi jana
No comments:
Post a Comment