
Wanyama ambaye amekuwa akitafutwa na klabu kadhaa kubwa zikiwemo Manchester United , Liverpool na Arsenal amekuwa akicheza kwenye kiwango cha juu hali ambayo imemfanya kuwa moja ya wachezaji waliotajwa sana kwenye dirisha la usajili mwaka huu .
Celtics imefikia makubaliano ya kumuuza Wanyama kwenda Southampton ambapo dili la kusajiliwa kwa mchezaji huyo litakamilika mara atakapopimwa afya yake pamoja na kukubaliana baadhi ya masuala binafsi kwenye mkataba wake.

Wanyama ni mdogo wa mchezaji mwingine toka Kenya McDonald Mariga anayecheza soka lake nchini Italia Kwenye klabu ya Parma na amewahi kuzichezea Inter Milan pamoja na Real Sociedad ya Hispania . Endapo usajili huo utakamilika Itakuwa historia nyingine kwa familia ya Mariga ambayo iliweka Historia pale McDonald alipocheza mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa mwaka 2010 ambapo alikuwa mchezaji wa kwanza toka Kenya na Afrika Mashariki kwa kizazi cha sasa kucheza fainali na kuvaa medali ya michuano hiyo .
Southampton itamnunua Wanyama kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 12.5 ada ambayo itamfanya Wanyama kushikilia rekodi nyingine ya kuwa mchezaji ghali kuliko wote kwenye ligi kuu ya soka ya Scotland na klabu ya Celtic.

No comments:
Post a Comment