facebook likes

Wednesday, July 10, 2013

Chidy Benz azuia kutoka kwa video ya ngoma aliyoshirikishwa


972201_584553924917440_1798184707_n
Hivi karibuni  msanii Baghdad ambaye alikuwa na umbo kubwa sana na kupungua ghafla, alitoa ngoma yake mpya akishirikiana na wasanii wawili ambao inasemekana kwamba hawana mahusiano mazuri. Wasanii hao ni Chidy Benz na Ney wa Mitego, kwa pamoja walishiriki kwenye ngoma moja ya Baghdad bila kujua kama wapo kwenye ngoma moja. Baadaye kutokana na  ratiba zao tofauti wakafanya video siku tofauti na katika location tofauti lakini kwa ajili ya ngoma moja hiyohiyo. Baghdad baada ya kuachia audio yake ambayo ilipata attention baada ya kusikika kwamba Ney wa Mitego na Chidy Benz wapo kwenye ngoma moja.
Habari kutoka kwenye chanzo cha uhakika zinasema kwamba Chidy Benz kutokana na kutokuwa na taarifa juu ya collabo hiyo, amepiga stop kutoka kwa video yake. Source ya story hii inaendelea kuhabarisha kwamba kuna mazungumzo yanafanyika na Chidy Benz kupata njia nzuri ya kuitoa video hiyo baada ya kuweka mambo kadhaa sawa kwenye maongezi hayo.


1044191_580378118668354_1069630180_n
Chidy Benz akiwa Maisha Club ambayo ni location iliyotumika kufanya video hiyo kwenye part ya Chidy.

1044861_580381218668044_2084355953_n
Ney wa mitego akiwa location Mbezi kwenye sehemu ambayo ili-rekodiwa part ya verse yake
Kama ulikuwa haujawahi kusikiliza ngoma yenyewe mtu wangu wa nguvu, chukua nafasi ya kusikiliza hapa

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...