facebook likes

Wednesday, July 10, 2013

KALI YA LEO: TIMU KUANDIKA MAJINA YA AKAUNTI RASMI ZA TWITTER ZA WACHEZAJI KWENYE JEZI ZAO




Klabu ya soka ya nchini Ubelgiji Zulte Waregem imetoa taarifa kwamba majina ya akaunti rasmi za mtandao wa Twitter za wachezaji wa timu hiyo zitakuwa zikiwekwa kwenye jezi zao kuanzia msimu ujao wa ligi unaotarajiwa kuanza hivi karibuni. 
Klabu hiyo imetoa tangazo hilo wakati ikitambulisha jezi mpya kwa ajili ya msimu wa 2013-14. Majina ya akaunti rasmi za Twitter za wachezaji yataandikwa kwenye kaptura. 
Zulte Waregem ilimaliza nafasi ya pili katika ligi ya msimu uliopita, nyuma ya mabingwa Anderlecht. Nafasi hiyo iliwatosha kuwapa nafasi ya kushiriki katika michuano ya mabingwa wa ulaya msimu ujao 

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...