facebook likes

Wednesday, July 10, 2013

Hii ndio TV inayouzwa milioni 24 dukani Dar es salaam

.
.
Kwenye duka la wakala wa Samsung Mlimani City Dar es salaam unaambiwa moja kati ya TV zenye gharama kubwa kuwahi kununuliwa ni hii kubwa kabisa ya sasa hivi ambayo ina inch 75, bei yake ni milioni 24….. kwa teknolojia yake unaweza kuwa unaangalia chochote kwa kutumia miwani za 3D.
Pia ina smart content, una create account na kupata applications kibao, ni tv ambayo unaweza ku-update yani kama Samsung wakileta teknolojia nyingine kwenye Tv hutatakiwa kununua Tv nyingine bali unatakiwa kununua kadi na ku-update hiyo teknolojia mpya.
Tv ya bei ndogo kuliko zote kwa Samsung sasa hivi ni inch 19 inayouzwa laki nne na nusu ambapo Tv zinazonunuliwa na Watanzania wengi ni za inch 32, 26, 40, na 46 ambayo ni smart TV unayoweza kuitumia pia kwa kutumia Internet.
.
.
.
Hii ndio TV kubwa kuliko zote za Samsung ambayo ina inch 75, yani bei yake ya milioni 24 ni pesa ambayo kama una kipato cha shilingi elfu 30 kwa siku, kuweza kuinunua inabidi usile wala kunywa au kufanya chochote kwenye hiyo elfu 30, uikusanye kwa siku mia nane (800)
.
.
Baada ya kukupa hiyo info kutoka Dar es salaam, kwa sasa zichukue hizi info nyingine kuhusu historia ya TV duniani…
1. Mwaka 1926 J.L BAIRD alitengeneza TV ya kwanza ambayo uwezo wake wa kuonyesha ulikua wa kiwango cha mistari 30 tofauti na TV za sasa zenye mistari mpaka 1080 ambayo ni high definition.
2.TV ya Panasonic ya Inch 150 ndio TV kubwa kuliko zote kwa sasa ambayo gharama yake ni dola laki moja za Kimarekani sasa hivi, pesa ambayo kibongobongo ni zaidi ya milioni 150.
3.Tangazo la kwanza kwenye TV liliruka hewani kwa mara ya kwanza siku ya kwanza ya July mwaka 1941 na lilihusu mechi ya mpira wa Baseball Marekani kati ya B. DODGERS NA PHILADELPHIA PHILLIES na lilikua la sekunde 20, gharama yake wakati huo ilikua dola 9 za Kimarekani ambayo kwa bongo ni zaidi ya shilingi elfu 10.
4.Kwa Marekani, watoto mpaka kufikia umri wa miaka 14 wanakua wameshuhudia matukio elfu kumi na moja ya mauaji kupitia TV.
5. Kipindi cha miaka ya 1950 kilifahamika kama zama za dhahabu kwa Televisheni, ni wakati ambapo matangazo ya kwanza ya rangi yaliruka, kabla ya hapo yalikua yanaruka ambayo ni black and white.
6.Remote ambazo hutumika kubadilishia channel na vitu vingine kwenye TV zilianza kutumika kwenye miaka ya 1980.
7. Matukio yaliyoweka rekodi ya kutazamwa sana kwenye TV ni michezo ya Olympic na michuano ya FIFA ya kombe la dunia.
8. Mwishoni mwa vita kuu ya pili ya dunia, Televisheni iligeuka kuwa rahisi kwenye umiliki kwa yeyote anaeweza kumudu gharama za kuinunua.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...