facebook likes

Thursday, October 10, 2013

Wachezaji watano kutoka Afrika watakaocheza ligi ya NBA 2013/2014


NBA Hasheem_Thabeet


Hasheem Thabeet (Tanzania)
Ndio mchezaji mrefu kuliko wote kwenye ligi ya NBA kwa sasa, majuzi wakati timu yake ya Oklahoma City Thunder ikicheza na Charlotte Bobcats Hasheem alicheza vizuri akiwa na point 13 alizofunga pamoja na kudaka Rebounds 10, huu utakua msimu wake wa pili akiwa na OKC.
SOMA ZAIDI.....

NBA Gorgui_DiengGorgui Dieng (Senegal)
Dieng (23) amesajiliwa na Minnesota Timberwolves baada ya kufanya vizuri akiwa na timu ya Louisville Cardinals inayoshiriki ligi ya vyuo vikuu Marekani NCAA.
NBA Ike_DioguIke Diogu (Nigeria)
Ike ni mchezaji wa kiafrika ambae amewahi kucheza ligi ya NBA kwa muda mfupi kabla ya kwenda barani Asia alikochezea timu ya XINJIANG FLYING TIGERS, GUANGDONG SOUTHERN TIGERS na timu mbili za PUERTO RICO ambazo ni CAPITANES DE ARECIBO na LEONES DE PONCE ila kwa sasa anarejea kwa mara ya pili kwenye ligi ya NBA ambapo atachezea timu ya NEW YORK KNICKS.

NBA Bismack_BiyomboBismack Biyombo (DRC)
Unaambiwa moja ya majina makubwa kwenye mchakato wa kuchagua wachezaji wanaotoka vyuoni mwaka 2011 lilikua jina la Bismack Biyombo ambae alichaguliwa na timu ya SACRAMENTO KINGS na mwaka huu amesajiliwa na CHARLOTTE BOBCATS ambako atakua akishindana kutafuta namba na Cody Zeller aliyejiunga na timu hiyo msimu huu.
BASKETBALL-SENEGAL-ANGOLA-FINALCarlos Morais (Angola)
Carlos Morais amesajiliwa kuichezea TORONTO RAPTORS msimu huu akiwa na uzoefu wa kuiongoza Angola kwenye mashindano kadhaa ya kimataifa na amewahi kucheza kwenye mashindano ya FIBA Afrika 2005 na 2007, mashindano ya dunia mwaka 2006 pamoja na mashindano ya Olimpiki mwaka 2008.
Kwa ripoti kama hizi, Breaking News na mengine ungana na mtu wako wa nguvu Millard Ayo na kuwa mwanafamilia wa millardayo.com kupitia facebook.com/millardayo twitter.com/millardayo na instagram.com/millardayo
Ripoti hii imeandaliwa na dstv.com ambayo hutoa habari za burudani kutoka kila kona ya hii dunia… unaweza kuwa unapita kwao kila siku mtu wangu…

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...