facebook likes

Thursday, October 10, 2013

Lenox Lewis kurudi ulingoni?

lewis

Bondia Muingereza Lenox Lewis huenda akareja ulingoni miaka kadhaa baada ya kustaafu mchezo huo .
SOMA ZAIDI....

Lennox ambaye mara ya mwisho alistaafu akiwa bingwa asiyepingwa wa masumbwi ya uzito wa juu ameshawishiwa kurudi ulingoni na mapromota toka Urusi ambao wanataka kuandaa pambano baina yake na Vittali Klitschko .
Mapromota wa Bondia wa Ukraine Vitali Klitschko ambaye pia ni mwanasiasa wanataka Lenox Lewis arudiane na Klitschko baada ya kumshinda wakati walipopambana mwaka 2003.
lenox
Hii ilikuwa mwaka 2003 wakati Lenox Lewis alipomchapa Vitali Klitschko kwa Knock Out .
Hata hivyo Lennox amesema kuwa anataka kupambana na mdogo wa Vitali ambaye ni Wladmir Klitschko lakini atakubali kurudi ulingoni endapo atahakikishiwa malipo ya dola milioni 100 .
Mapromota toka Urusi wameahidi kumpa Lenox dola milioni 50 lakini kuna mazungumzo ambayo yanaendelea na kuna uwezekano wad au hilo kuongezeka .
Wladmir Klitschko ambaye Lenox Lewis anataka kupambana naye.
Wladmir Klitschko ambaye Lenox Lewis anataka kupambana naye.
Lennox Lewis alimchapa Vitali Klitschko kwa Knock Out ya raundi ya sita wakati wawili hao walipopambana mwaka 2003 .
Wanandugu wa familia ya Klitschko Wladmir na Vitali wamekuwa wakitawala mchezo wa masumbwi kwa muda mrefu na hakuna bondia yoyote ambaye ametokea kuleta upinzani kwao.
Lennox Lewis amesema kuwa anahitaji miezi sita ya kurudi kwenye kiwango chake na anaamini anaweza kumshinda Wladmir endapo watafikia makubaliano ya kupanda ulingoni.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...