Ilikuwa rahisi kumuita Besta na ukaishia hapo lakini kwa sasa unaweza kumuita Mrs. Marlaw, baada ya ukimya wa muda mrefu na kisha kuachia wimbo wa ‘For My Baby’ ambao ni dedication kwa mmewe na baadae akakaa kimya, amewakumbusha fans wake kuwa bado yupo na atakuja tena kimuziki.
SOMA ZAIDI..........
Besta amefunguka kupitia kipindi cha Bongo Dot Home cha 100.5 Times Fm wakati akipiga story na Moko Biashara na Jabir Saleh, “Muziki ni kazi yangu na nimeihangaikia sana...nawaambia mashabiki wangu kwamba nipo na ntarudi tena kimuziki na nawashukuru sana kwa sapoti yao na nawapenda sana.”
‘Baby Boy’ hit maker ambae ni mama wa mtoto Starence, amezungumzia pia kuhusiana na wasanii ambao wamejiingiza katika madawa ya kulevya na akatoa ushauri.
“Kwenye madawa ya kulevya kwa kweli inasikitisha, lakini nawapongeza wasanii ambao walikuwa wameingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya lakini wameweza kutoka, na wanaweza kuwahamasisha wengine ambao ni wanga kuwa inawezekana kutotumia madawa ya kulevya ama wanaweza pia kutoka. Lakini pia inasikitisha kusikia wanasema kwamba wanamuziki wengi wanatumia madawa ya kulevya, ni vizuri wakafahamu kuwa muziki bila kutumia madawa ya kulevya inawezekana, unaweza kufanya muziki bila kutumia madawa ya kulevya na ukafanya muziki mzuri. Kikubwa ni kwamba tusijihusishe na madawa ya kulevya kwa sababu sio kitu kizuri, na tumeshasikia mfano kutoka kwa watu ambao walikua wakitumia na yakawaharibu.” Amesema Besta.
Amewashauri pia wasanii ambao kwa sasa wako juu kwenye game, “nachoweza kuwaambia ni kwamba unapokuwa kwenye pic usijisahau na inabidi uendelee kujitahidi kufanya vitu vizuri zaidi ili uendelee kuwa kwenye pic, na kuwapenda washabiki kwa kuwa bila wao..wao ndo kila kitu.

No comments:
Post a Comment